Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi (wa kwanza kushoto), akimsikiliza mwananchi huyu aliyetembelea katika banda la PSSSF leo Julai 2, 2020. Katikati ni Bw. Meseka Kadala, Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
**
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema katika msimu huu wa maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam unatoa huduma kamili kama ambazo zinazopatikana kwenye ofisi zake kote nchini.
Akizungumza na kwenye banda namba 13 la Mfuko huo
kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam , Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi amesema kwa mantiki hiyo Mfuko umewaalika wanachama wa Mfuko na wananchi kwa ujumla
kufika katika banda hilo ili kujipatia huduma na taarifa mbalimbali.
“Tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kutembeela banda letu kwani huduma zote za kiofisi ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini
zinapatikana hapa”, alisema Bw. Abdul Njaidi.
Alitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na mwanachama kupata taarifa kuhusu Pensheni, Mafao, uhakiki, uwekezaji na taarifa za michango.
Katika hatua nyingine, Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uendelezaji Bishara Tanzania (TANTRADE), Bi. Theresa Chilambo amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
anatarajiwa kuyafungua rasmi maonesho hayo Ijumaa Julai 3, 2020.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw.Donald Maeda (kushoto), akimsikiliza mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF ili kupata taarifa za michango yake.
Wanachama wa PSSSF wakihudumiwa kwenye banda la Mfuko huo leo Julai 2, 2020.
Afisa Huduma kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Bi. Nelusigwa Mwalugaja (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo Julai 2, 2020.
Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi (wa kwanza kushoto) na Afisa Uhusiano wa Mfuko huo Bw. Meseka Kadala, wakiwasikiliza wananchi hawa waliohitaji kuhudumiwa Julai 2, 2020.
Afisa Mafao PSSSF, Bw. Abdallah Juma Adam (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa PSSSF aliyefika kwenye banda la Mfuko huo, Julai 2, 2020.
Afisa Matekelezo Mwanzamizi wa PSSSF, Bi. Zainab Ndullah (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo Julai 2, 2020.