Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza kubadilisha jina la Uwanja wa Taifa na kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium kama sehemu moja wapo ya kumuenzi marehemu Mkapa.
Rais amesema ameona maoni mengi ya watu kutaka uwanja huo uitwe jina la Mkapa hivyo na yeye ameridhia
“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium.
“Hata kwenye Michezo alitoa mchango tena nasikia alikuwa mshabiki mkubwa wa Yanga, ingawa sikuwahi kumsikia akisema hilo hadharani, Mzee Kikwete hapa ansema ni kweli kwa sababu na yeye ni Yanga, sifahamu Mzee Mwinyi yeye ni timu gani” Amesema Rais Magufuli
Social Plugin