Rais wa Urus Vladimir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kubakia madarakani hadi 2036.
Putin mwenye umri wa miaka 67, amekuwa madarakani kama rais na pia waziri mkuu kwa miongo miwili na kwa hivi sasa ni rais aliyedumu nchini Urusi kwa kipindi kirefu zaidi
Kura ya maoni ilitaka kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba ambayo yatamuwezesha Putin kugombea tena katika uchaguzi mara mbili zaidi na kuweza kubakia madarakani hadi akiwa na umri wa miaka 83. Muhula wake wa hivi sasa unamalizika miaka minne ijayo. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Urusi Ella Pamfilova amesema.
Putin amejijengea umaarufu kuwa ni mlinzi na kiongozi anayeweza kuleta uthabiti nchini humo, kinyume na hali ya kuyumba kwa uchumi na kisiasa katika kipindi baada ya iliyokuwa jamhuri ya kisovieti katika miaka ya 1990 ambayo imekuwa kabla ya kuingia kwake madarakani.
-DW