RC MBEYA, ALBERT CHALAMILA ATENGUA UAMUZI WAKE WA KUGOMBEA UBUNGE


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema kuwa hawezi kukiuka maagizo ya Rais Magufuli aliyowataka wateule wake kuridhika na nafasi walizonazo, hivyo ameamua kuendelea kuwatumikia wananchi wake na hivyo hawezi tena kukimbilia kugombea Ubunge.


“Nilikuwa miongoni mwa watia nia ya kugombea ubunge Iringa mjini, kwa sasa sintofanya hivyo zaidi ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mbeya na kutii maelekezo ya Rais Magufuli,” amesema Chalamila  na kuongeza;

 "Ni hekima na busara na itakuwa ni utoto wa kupindukia kama leo hii nitakwenda kuchukua fomu kugombea nikashinda kwenye kura za maoni, halafu huku Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi nimekwishamkwaza kwa kuwaacha Watanzania wake wakilia na kuhangaika".  

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne tarehe 7 Julai 2020 jijini Mbeya  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari  na kuongeza kuwa kuna miradi mingi amepewa kuisimamia, hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu kuukimbia Ukuu wa Mkoa na kukimbilia Ubunge, huku akiacha miradi hiyo bado haijakamilika.

Wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma Rais Magufuli alisema ili kazi ziendelee, taifa lazima liendelee kutatua matatizo ya  kila siku ya wananchi, hivyo alisema  hawezi kusubiri mtu anayeomba ruksa  ya kusaka ubunge, akakose ndo arudi tena.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post