Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : CCM SHINYANGA YASHTUSHWA KASI YA UTOAJI RUSHWA WAGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI…YAKUTANA NAO KIKAO CHA DHARURA KUWAONYA



Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini na kuwatahadharisha kuhusu mienendo ya baadhi ya wagombea kutoa rushwa ili wachaguliwe kuwa wagombea ubunge.




Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Katika kile kichoonekana kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechoshwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wa nafasi za Uongozi, CCM mkoa wa imeitisha kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini na kuwatahadharisha kuhusu mienendo ya baadhi ya wagombea kutoa rushwa ili wachaguliwe kuwa wagombea ubunge.



Akizungumza katika kikao hicho cha dharura kilichofanyika leo Julai 18,2020 majira ya saa tano na robo asubuhi, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema kama wagombea hao wa ubunge wataendelea kujihusisha na vitendo vya rushwa Chama Cha Mapinduzi kitafuta majina ya walioomba kugombea ubunge.



Magesa ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye amekutana na wagombea hao kutokana na Agizo la Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally amekemea vitendo vya rushwa kwa wagombea kwani uchaguzi huo na kwamba atakayetoa rushwa chama kitamshughulikia kwani uchaguzi ni wa haki hauhitaji kutumia fedha ili uchaguliwe kuwa kiongozi.

“Kutafuta fedha,kutafuta wapiga kura na kuwapa chochote ni marufuku kuanzia sasa. Kuanzia sasa fanya kazi zako fanyia nyumbani kwako, na hao mawakala mnaowatuma kwenda kugawa fedha tutawakamata. Na tutafuta uchaguzi. Hapo mlipofikia kugawa nasema sasa marufuku, sitaki kusikia mgombea anajihusisha na vitendo vya rushwa. Mkiendelea tutagawa fomu upya za kuomba kugombea ubunge na hamtaruhusiwa kugombea”,amesema Magesa.

“Niwaombe sana ndugu zangu kama umeingia kutafuta kura watu watakufahamu, usiende kushawishi,hao mawakala wenu tutawashika. Baadhi yenu wanatoa rushwa, ni uchaguzi wa aina gani huo?. Mnaenda kununua kura kwanini??,mnatembelea watu kwanini? Hiki mnachofanya Shinyanga Mjini ni fujo..Naomba kugawa fedha kuishe,kugawa vitenge kuishe”,amesema Katibu huyo wa CCM.

“Kushinda kura za maoni siyo kuteuliwa kugombea, tuna vigezo zaidi ya 15 vinavyomfanya mtu ateuliwe kugombea Ubunge. Unaweza kuongoza kura za maoni lakini usiletwe. Hapo mlipofikia panatosha, mistake kuharibu uchaguzi. Mkiendelea kutafuta kura kwa kutembelea miji ya watu kutoa rushwa tufatuta uchaguzi, tutafuta majina yote. Ikishindikana tutaleta hata wagombea wengine ambao hawakuomba kugombea",ameongeza Magesa.

Magesa amemuagiza Katibu wa wilaya ya Shinyanga Mjini kuwaandikia barua ya maagizo wagombea kufanya uchaguzi kwa ustaarabu,kutofanya kampeni wasubiri siku ya mkutano wa kura za maoni utakaofanyika Julai 20,2020.

"Umoja ndiyo ushindi wetu, tushirikiane kujenga chama. Sisi tunatafuta mtu atakayekivusha chama, tunataka mtu anayependeka kwa wananchi wa Shinyanga, sikieni sauti za wananchi kuwa wanataka nani awe mbunge wao",ameongeza.

Jumla ya wanachama 60 wa CCM wamechukua na kurudisha fomu kuomba kugombea Ubunge Shinyanga Mjini ambapo mkutano wa kuwapigia kura za maoni utafanyika Julai 20,2020.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akikemea vitendo vya rushwa kwa wagombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na kwamba atakayetoa rushwa chama kitamshughulikia.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.

Wanachama wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.


Wanachama wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.



Viongozi wa CCM wakiwa kwenye kikao hicho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com