Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya wanachama 60 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini katika zoezi la uchukuaji fomu lililoanza Julai 14,2020 na kuhitimishwa leo Julai 17,2020 majira ya saa 10 jioni.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga amesema kati ya wanachama 60 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu, wote wamerudisha wakiwemo wanawake ni saba na wanaume 53.
Bwanga amesema Mkutano wa kura za maoni kuwapigia kura wagombea utafanyika Julai 20,2020.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Emmanuel Lukanda amesema jumla ya wanachama 54 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa ambapo kati yao wanawake ni wanne na wanaume ni 50.
Kwa upande wa Jimbo la Kishapu jumla ya wanachama 78 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge ambapo kati yao wanawake ni wanne na wanaume ni 74.

Social Plugin