Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU MANYARA YAFANIKIWA KUREJESHA FEDHA ZILIZOPORWA NA MKUU WA SHULE

Na John Walter-Babati

Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoani Manyara imefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni nne za watumishi wa shule ya msingi Birsima, ambazo zilifanyiwa ubadhirifu na Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo, Aman Paul Mkeni.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Holle Makungu imesema Fedha hizo zimekabidhiwa kwa wahusika na afisa wa TAKUKURU  dawati la Udhibiti Bi.Edda Senkondo  juni 30,2020.

Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Manyara Holle Makungu, amesema Mkeni ambaye pia ni Mhasibu wa shule hiyo iliopo wilayani Babati, alishindwa kutimiza wajibu wake wa kuwalipa fedha hizo watumishi hao wasio walimu na kuzifanyia ubadhirifu.

Watumishi Waliokabidhiwa fedha zao kwenye mabano ni Ezekiel Rory (410,000), Daniel Jacob (1,400,000) na Melania Bayo (300,000).

Amesema wamefanikiwa kurejesha fedha hizo baada ya kupata malalamiko ndipo walipomtaka Mwalimu Mkeni  kuwasilisha fedha hizo.

Hata hivyo Makungu ameshauri uongozi wa shule hiyo umpe mwalimu mwingine mwenye uadilifu kazi ya kutunza fedha kwa kuwa Mwalimu huyo hastahili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com