Mhandisi Mtafiti wa TANESCO, Aurea Bigirwamungu akitoa Elimu kwa Wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi uliyopo wilayani Bahi juu ya matumizi bora ya Umeme
Mhandisi Mtafiti wa TANESCO, Aurea Bigirwamungu akisisitiza jamboa wakati wa kutoa Elimu kwa Wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi uliyopo wilayani Bahi juu ya matumizi bora ya Umeme
Afisa Masoko TANESCO,Adelina Lyakurwa akizungumza na wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi(hawapo pichani) uliyopo wilayani Bahi wakati wa kutoa elimu juu ya matumizi bora ya Umeme
Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja TANESCO Dodoma, Mariam Juma akieleza faida ya nishati ya umeme kwa wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi (hawapo pichani) wakati wa kutoa elimu kwa juu ya matumizi bora ya umeme leo Wilayani Bahi
Baadhi ya Wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi waliyojitokeza kupatiwa elimu juu ya matumizi bora ya Umeme kutoka kwa watendaji wa TANESCO leo Wilayani Bahi.
Afisa Masoko TANESCO Adelina Lyakurwa akiwa na Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja TANESCO Dodoma Mariam Juma wakionyesha kifaa cha umeme(umeter) kwa wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi wilayani Bahi.
Katibu wa Mgodi wa Dhahabu wa Nholi Sebastian Aloyce (wakwanza kushoto) akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi huo na pembeni yake ni Meneja Mgodi Kulwa Limbu akimsikiliza kwa makini.
Watendaji wa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika Mgodi wa Nholi uliyopo wilayani Bahi baada ya kupatiwa elimu ya matumizi bora ya nishati ya Umeme.
Mhandisi Mtafiti TANESCO Aurea Bigirwamungu akikagua baadhi ya mitambo ya wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu wa Mgodi wa Nholi wilayani Bahi .
Wachimbaji wadogowadogo wa Mgodi wa Nholi wilayani Bahi wakiwa katika shughuli zao za uzalishaji.
Mwonekano sehemu moja wapo ya eneo la Mgodi wa Dhahabu wa Nholi wilayani Bahi
……………………………………………………….
.
Na. Alex Sonna, Bahi
Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi wa Nholi wilayani Bahi kupatiwa nishati ya umeme ndani ya miezi sita ili kuongeza uzalishaji katika mgodi huo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhandisi Mtafiti Aurea Bigirwamungu wakati wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogowadogo na wakazi wa kata hiyo kwa ajili ya matumizi bora ya umeme.
Mhandisi Bigirwamungu amesema kuwa mradi wa kuwafikishia nishati ya umeme wakazi hao utatekelezwa ndani ya miez sita ili kurahisisha shughuli za wajimbaji hao hasa katika uchenjuaji wa dhahabu na shughuli nyingine katika mgodi huo.
Aidha Mhandisi Bigirwamungu amesema kuwa wachimbaji hao shughuli zao nyingi zinahitaji nishati ya umeme ili kuongeza uzalishaji katika ujimbaji wa dhahabu ambapo nishati hiyo itaweza kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Ninaimani kubwa ndani ya miezi sita mradi huu utatekelezwa na kukamilika hivyo wakazi wa hapa watanufahika na kuongeza chachu katika uzalishaji na maendeleo yao ” ameweka wazi Mhandisi Bigirwamungu.
Lakini pia Mhandisi Bigirwamungu amesisitiza kuwa baada ya elimu hiyo wachimbaji hao wahakikishe wanatumia vifaa vilivyo bora hasa ambavyo havitumii umeme mwingi , lakin pia kuwa na matumizi mazuri ya umeme kila baada ya matumizi kuzima umeme huo.
Naye Afisa Masoko Adelina Lyakurwa ametoa wito kwa wakazi hao kuchangamkia fursa ya kupata nishati ya umeme ili kuongeza uzalishaji katika shughuli zao za uchimbaji.
“Hivyo basi taratibu za kufanikiwa kupatiwa umeme ni kuhakikisha unapata fomu ya kuomba kupatiwa umeme, ukisha jaza fomu hiyo isainiwe na mkandarasi alafu irudishwe TANESCO na fanya kutandaza nyaya katika nyumba yako muda ukifika basi wewe ni kufungiwa umeme” amebainisha Lyakurwa.
Aidha Lyakurwa ameongeza kwa Nishati hii ya umeme kwa wakazi hao wataunganishiwa nishati ya umeme kwa shilingi 27,000 tu.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja TANESCO Dodoma Mariam Juma ameweka wazi kuwa lengo la kuwasogezea nishati ya umeme wakazi hao ni kuhakikisha wanatumia nishati hiyo kuchenjua dhahabu na shunguli nyinginezo katika mgodi huo ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo na kuleta maendeleo kwa ujumla.
Pia Mariamu amewashukuru wakazi wa kata hiyo kwa mwitiko waliyowapa na kusema kuwa elimu waliyopatiwa itakwa na manufaa kwao na kuleta tija kwao.
Kwa niaba ya wachimbaji na wananchi wa kata hiyo Meneja mgodi Kulwa Limbu ametoa changamoto ya wachimbaji hao kuwa wamekuwa wakitumia dizeli katika shughuli zao za uzalishaji wa dhahabu ambayo imekuwa ikuuzwa kwa bei ghali na kusababisha shughuli za mgodini kutotekelezwa ipasavyo.
“Sisi tuko tayari kutumia nishati ya umeme hivyo nitoe wito kwenu watendaji wa TANESCO kuwa mradi huo uweze kukamilika ndani ya muda mliosema ili tuweze kunufaika na mradi huo kwa kuongeza uzalishaji ” ametoa rai