Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara leo amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini.
Nyerere Jackson Mwera akichukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini
Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Tarime.
Wanachama 42 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini kupitia CCM huku idadi ya wanawake ikiwa ndogo ikilinganishwa na wanaume.
Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime mkoani Mara,Hamis Mkaruka amesema kuwa hadi kufikia siku ya leo Julai 15, 2020 wanawake waliochukua fomu ni watano pekee ,wanaume wakiwa 37.
Mkaruka alisema kuwa kwa upande wa Jimbo la Tarime mjini wanawake ni Suzy Chambili,Monica Anicet na Dr.Veronica Robert ambapo Jimbo la Tarime vijijini ni Joyce Ryoba na Dr. Stella Faustine
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Mwikwabe Waitara amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini.
Makada wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge hadi kufikia siku ya leo majira ya saa nane mchana waliochukua fomu jimbo la Tarime vijijini ni 24 na Tarime mjini wakiwa 18 .
Wengine waliochukua fomu kwa jimbo la Tarime mjini ni Hezbon Mwera, Jackson Ryoba, Dr.Edward Machage,Julius Mtatiro Eng.William Machage,Cheche Andrew,Julius Labaran,Samwel Marwa,Evangel Otieno,Michael Kembaki,Jeremia Seba,Gerald Martine,Mwita Joseph,Zakayo Wangwe na Manchare Heche Siguta.
Kwa jimbo la Tarime vijijini ni Joseph Nyahende,Yusuph Wambura,Chacha Masero,John Gimunta,Mwita Jacob Marwa,Wambura Sagire,Thomas Chacha Mwita, Musa Raphael, Nyerere Mwera,Nyamhanga David,Dr.Abdalah Chigo,Dr.Paul Mwikwabe,Mordikae Moset,Eliakimu Maswi,Nicodemas Keraryo,James Bwire,Peter Amos Bhusene Frank Mniko,Lucas Magoti,Samwel Mantarya na Ngocho Darius.
Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka alisema kuwa wanawake wanapaswa kuondoa hofu na badala yake wajitokeze kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.
Social Plugin