Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amechukua fomu ya kugombea urais wa Tanzania, kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
Fomu hiyo imechukuliwa leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam na wakala wa Lissu David Jumbe
“Nimekuja kwa ajili ya kuchukua fomu kama wakala wa Tundu Lissu, mnafahamu Lissu yuko nje ya nchi.
“Tukitoka hapa, tutaanza kazi ya kujaza na kutafuta wadhamini na kwa mujibu wa maelekezo, tupate wadhamini 100 kwa kila kanda. Tukitoka hapa tutaanza Kanda ya Pwani,” amesema Jumbe.
Social Plugin