Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema mwishoni mwa mwezi Julai, 2020 atarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kisiasa.
Amesema, atafanya hivyo ili aweze kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 Julai 2020.
Mikutano hiyo, pamoja na mambo mengine, itampitisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
Mchakato wa uchakuaji na urejeshaji fomu za kuwania Urais wa Tanzania unaanza leo Jumamosi tarehe 4 hadi 19,2020.
Wagombea au mawakala wao watakuwa na fursa ya kuchukua fomu kisha kutafuta wadhamini 100 katika kila kanda kumi za chama hicho.
Lissu ni miongoni mwa wanachama ambao wamekwisha tia nia hadharani ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki.
Social Plugin