TVMC YAKUTANA NA VIONGOZI WA KAMATI ZA MTAKUWWA KATA 7 ZA HALMASHAURI YA SHINYANGA

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Adriana Leonard akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Julai 17,2020.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC) Shinyanga limeendesha kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kujadili na kuangalia matokeo yaliyotokana na utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kikao hicho kimefanyika leo Ijumaa Julai 17,2020 katika Ukumbi wa Hoteli ya Karena Annex na kukutanisha pamoja viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata za Samuye, Usanda, Tinde, Nsalala, Didia, Masengwa na Ilola ambako TVMC inatekeleza Mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa ufadhili wa shirika la Foundation For Civil Society.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Adriana Leonard amesema mpaka sasa shirika hilo limewezesha uanzishwaji wa kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata katika kata hizo saba ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya utekelezaji wa MTAKUWWA.

“Shirika la TVMC pia limewezesha kuratibu mchakato wa uanzishwaji wa sheria ndogo ndogo zinazopinga ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa na mimba za utotoni katika kata hizo”,amesema Adriana.

Amesema kikao kilikuwa na lengo la kujadili na kuangalia matokeo yaliyotokana na utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kutokana na shughuli zilizotekelezwa kwa kushirikiana na watendaji ngazi ya kata na halmashauri tangu mradi huo ulipoanza mwaka 2018 utaokamilika Desemba 2020.

Kwa upande wao Viongozi hao wa kamati za MTAKUWWA wamesema matukio ya ukatili wa kijinsia hususani yale ya mimba na ndoa za utotoni yamepungua kwa kiasi kikubwa huku wakieleza kuwa matukio ya utekelezaji familia yameendelea kuwepo katika jamii.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Adriana Leonard akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Julai 17,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Adriana Leonard akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Usanda, Halima Tendega akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Usanda kwenye kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Tinde Eva Mlowe akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Tinde kwenye kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa Mtendaji kata ya Samuye, Damian Ndassa akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Samuye kwenye kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Masengwa, Remicius Tirumanyika akiwasilisha taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Masengwa kwenye kikao cha viongozi wa kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Viongozi wa kamati za MTAKUWWA kwenye kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post