Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SULEIMAN NCHAMBI ARUDISHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KISHAPU...HADI LEO WALIOOMBA UBUNGE KISHAPU NI 59

Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu, Helena Chacha (kulia) akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Kishapu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi leo Julai 15,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Kishapu.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi leo Julai 15,2020 amechukua na kurudisha fomu ya kuomba kugombea tena Ubunge Jimbo la Kishapu katika ofisi za CCM wilaya ya Kishapu.

Suleiman Nchambi ambaye anatetea kiti chake ni miongoni mwa wanachama 59 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu, Helena Chacha amesema tangu jana hadi kufikia leo Jumatano Julai 15,2020 majira ya saa 10 jioni wanachama 59 wamefika ofisini kwake kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Kishapu kwa tiketi ya CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com