STEPHEN MASELE ASHINDA KWA KISHINDO KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA SHINYANGA MJINI




Stephen Masele akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 20,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkutano wa Maalumu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wa kupiga kura za maoni kupata mwanachama wa CCM atakayegombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020 uliofanyika leo Julai 20, 2020 katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga umemalizika ambapo Stephen Julius Masele aliyekuwa anatetea kiti chake ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.

Msimamizi wa Uchaguzi huo Joachim Simbila ambaye ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Kahama ametangaza matokeo kama ifuatavyo:

1.Stephen Julius Masele - kura 152
2.Jonathan Manyama Ifunda - kura  65
3.Gasper Kileo - kura 51

🔻🔻🔻🔻🔻🔻🔻
4.Erasto Kwilasa amepata kura 31
5. Mayunga Stanley Otto kura 20
6. Seni Abdallah Jacobo kura 17, 
7. Patrobas Katambi amepata kura  kura 12,
8.Busumabu Daudi kura 11
9.Mapesa Marco kura 8 
10.Alex Peter -5
11. Singu Andrew Stephen- 5
12.Makune Soso - 5

  Wagombea wengine wamepata kura chini ya nne huku wengi wakipata kura 1 na wengine 0.

Jumla ya wagombea 58 walikuwa wanachuana ambapo jumla ya wajumbe wa mkutano waliotakiwa kupiga kura ni 431 waliopiga kura ni 429 kura zilizoharibika ni  3  kura halali 426.

"Baada ya matokeo haya hakuna mshindi, hii ni hatua ya kwanza tu bado kuna michakato itafuatia. Si vyema mgombea atakayeonekana hana kura nyingi akazomewa...lakini si vyema kwa aliyepata kura nyingi akaenda kusherehekea..sherehe tutafanya baada ya chama kushinda",amesema msimamizi wa uchaguzi. 

Akizungumza baada ya kutangazwa kuongoza katika kura za maoni, Masele amewashukuru wajumbe wa mkutano kwa imani waliyompa kwa kumpigia kura nyingi huku akiuongeza uongozi wa CCM kwa kuweka taratibu nzuri za kusimamia uchaguzi huo kwa uwazi kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Masele aliwapongeza wagombea wenzake akiwemo Jonathan Manyama Gasper Kileo, Erasto Kwilasa kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu katika masuala ya siasa kwa kupitia mchakato wa kutafuta kura kwa ustaarabu wa hali ya juu huku akiwataka wageni waliogombea kwa mara ya kwanza wajifunze kutoka kwa watu hao kwani misingi ya CCM ni urafiki na undugu.



Msimamizi wa Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Shinyanga Joachim Simbila akizungumza kwenye Mkutano wa Maalumu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wa kupiga kura za maoni kupata mwanachama wa CCM atakayegombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Stephen Masele akiwashukuru wapiga kura wake kwa kumpa kura za kutosha
Stephen Masele akiwashukuru wapiga kura wake kwa kumpa kura za kutosha


Stephen Masele akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 20,2020



Wagombea wakiwa ukumbini.


Stephen Masele akienda kujipigia kura


Wajumbe wakiwa kwenye foleni kuchukua karatasi za kupigia kura


Wajumbe wakiwa kwenye foleni kuchukua karatasi za kupigia kura


Wajumbe wakiwa kwenye foleni kuchukua karatasi za kupigia kura


Wagombea ubunge wakisubiri matokeo


Zoezi la kuhesabu kura likiendelea


Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Jonathan Manyama Ifunda akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Erasto Kwilasa akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Gasper Kileo akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Salula Gacha akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Patrobas Katambi akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Stanley Otto Mayunga akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.


Peter Frank Alex ' Teacher Black' akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.


Eunice Jackson Wiswa akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.


Lydia Pius akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Musa Jonas Ngangala akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post