Azmina Arif Amir akionesha namba yake wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa kura za maoni Ubunge Viti Maalum Kupitia UVCCM Mkoa wa Shinyanga ambapo ameibuka mshindi wa 1 kwa kupata kura 13 kati ya kura 28 zilizopigwa akifuatiwa na Janeth Dutu kura 6 na Leah Mbeke kura 5.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Azmina Arif Amir ameibuka mshindi wa kwanza katika uchaguzi wa kura za maoni Ubunge Viti Maalum Kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga kwa kupata kura 13 kati ya kura 28 zilizopigwa huku Janeth Dutu akipata kura 6 na Leah Mbeke akipata kura 5.
Akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa Mkutano wa Baraza la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020 Msimamizi wa uchaguzi huo, Dkt. Philemon Sengati ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tabora amesema uchaguzi huo umekuwa wa huru na haki ambapo maamuzi zaidi yatatolewa katika Mkutano wa Baraza la Vijana UVCCM taifa.
Amewataja vijana 14 wa CCM waliojitokeza katika kinyang’anyiro cha nafasi ya ubunge viti maalum kupitia kundi la Vijana CCM kuwa ni Azmina Arif Amir ambaye amepata kura 13, akifuatiwa na Janeth Dutu aliyepata kura 6 na Leah Donald Mbeke aliyepata kura 5 akifuatiwa na Sikitu Elson Samwel kura 2,Suzana Reuben Jilili kura 1 na Jackline Emanuel Ndombile kura 1.
Wengine ni Cecilia Peter Mhande,Husna Salam Zahrani, Jesca Jumanne Masehese,Mercy Athanas Lukuba,Mercy Gasper Kyando,Prisca Lazaro Mawoo, Rebeca Boniphace Giti na Theresia Masanja ambao hawakupata kura.
“Mara baada ya kuchaguzi huu kama hapatakuwa na mapingamizi huyu mshindi tutampeleka katika hatua nyingine. Hapa tunahitaji mshindi mmoja tu atayewakilisha mkoa wa Shinyanga atayeingia kwenye kinyanganyiro kitaifa ili kupata wabunge sita Tanzania Bara",amesema Dkt. Sengati.
Tazama picha hapa chini
Tazama picha hapa chini
Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020. Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu,kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Kundi la Vijana CCM.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Kundi la Vijana CCM.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakionesha namba zao wakati za zoezi la kupiga kura.
Azmina Arif Amir akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Azmina Arif Amir akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Janeth Dutu akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM.
Leah Mbeke akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakipiga kura
Wajumbe wakipiga kura
Wajumbe wakipiga kura
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020.
Leah Mbeke akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka mshindi wa tatu kwa kupata kura 5
Janeth Dutu akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka mshindi wa pili kwa kupata kura 6
Azmina Arif Amir akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kupata kura 13
Azmina Arif Amir akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kupata kura 13.
Cecilia Peter Mhande akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Husna Salam Zahrani akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Jackline Emanuel Ndombile akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Jesca Jumanne Masehese akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Mercy Athanas Lukuba akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Mercy Gasper Kyando akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Prisca Lazaro Mawoo akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Rebeca Boniphace Giti akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Sikitu Elson Samwel akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Susani Reuben Jilili akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM
Theresia Masanja akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin