Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime Daud Ngicho akizungumza na Watia nia wa Ubunge
****
Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Tarime
Wanachama 56 wa CCM wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini ambapo kati yao 53 wamerudisha fomu.
Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime mkoani Mara,Hamis Mkaruka alisema kuwa katika Jimbo la Tarime Vijijini wanachama 30 wamechukua fomu na wote wamezirudisha na katika Jimbo la Tarime mjini waliochukua fomu walikuwa 26 lakini waliorudisha ni 23 na watatu hawakurudisha.
Mkaruka aliyasema hayo mbele ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuomba kugombea ubunge katika ukumbi wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime ambapo yeye na viongozi wa chama hicho waliwaonya kutotukanana,kuchafuana na kutotoa rushwa kama njia ya kushawishi wajumbe kuwapigia kura kwani kinachohitajika ni mtu kujieleza nini atakachokifanyia chama,Wanachama na wananchi.
"Mmerudisha fomu kugombea ni haki yako lakini kuteuliwa ni haki ya vikao uchaguzi utafanyika tarehe 21 mwezi wa saba,2020 na usidhani ukiongoza kwa kura nyingi wewe ndiyo mshindi bado kuna michujo mingine maana kuna watu humu ndani ya CCM wanafahamika lakini huko nje hawafahamiki tunataka mgombea mwenye sifa za kuku wa kienyeji kwakuwa yeye uacha mayai kwenye banda nakujitafutia mwenyewe mayai kuliko kuku wa kisasa anaengoja kutafutiwa chakula",alisema Mkaruka.
Katibu Mwenezi CCM wilaya ya Tarime Marema Solo alisema kuwa wana CCM ni familia moja hivyo ni lazima kuwa wamoja kwa maslahi ya chama nakwamba hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM wote ni wanachama sawa huku akiwakumbusha kusoma maandiko ya Biblia Mathayo7:7 kinachosema ombeni,nanyi mtapewa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime Daudi Ngicho alisema kuwa watia nia ni wengi na nafazi za ubunge kwenye wilaya ni mbili zinazohitaji watu wawili nakwamba atakayeshinda watia nia wengine wamuunge mkono kuhakikisha CCM Tarime inashinda majimbo yote mawili.
Ngicho alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakiwachafua wenzao kupitia mitandao ya kijamii huku akiahidi kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama lengo kuhakikisha CCM inapita kwa kishindo.
Aliwaonya kutotoa rushwa kwa wajumbe,watiania kutosafirisha wajumbe siku ya uchaguzi nakwamba chama ndicho kitasafirisha wajumbe kwenda katika kumbi zitakazotumika kufanya uchaguzi siku ya tarehe 21 mwezi huu nakusema kuwa Uchaguzi jimbo la Tarime mjini utafanyika ukumbi wa CCM wilaya na Jimbo la Tarime vijijini utafanyika ukumbi wa chuo cha ualimu.
Watia nia katika Jimbo la Tarime mjini ni Suzy Chambili,Monica Anicet,Dr.Veronica Robert, Hezbon Mwera, Jackson Ryoba, Dr.Edward Machage,Julius Mtatiro, Eng.William Machage,Cheche Andrew,Julius Labaran,Samwel Marwa,Evangel Otieno,Michael Kembaki,Jeremia Seba,Gerald Martine,Mwita Joseph,Zakayo Wangwe, Manchare Heche Siguta,Mwita James,Ditu Manko,Philip Nyirabu,Robert Mwitango,Justin Mugendi,Deogratius Meck,Segere Shadrack na Col.Kichonge Masero na miongoni mwao watatu hawakurudisha fomu.
Kwa jimbo la Tarime vijijini ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara, Joyce Ryoba,Dr.Stella Faustine, Joseph Nyahende,Yusuph Wambura,Chacha Masero,John Gimunta,Mwita Jacob Marwa,Wambura Sagire,Thomas Chacha Mwita, Musa Raphael, Nyerere Mwera,Nyamhanga David,Dr.Abdalah Chogo,Dr.Paul Mwikwabe,Mordikae Moset,Eliakimu Maswi,Nicodemas Keraryo,James Bwire,Peter Amos Bhusene, Frank Mniko,Lucas Magoti,Samwel Mantarya, Ngocho Darius,Pius Mawa,Harun Kihengu,Maseke Muhono na Dr.Edward Machage na wote wamerudisha fomu.
Watia nia wa Ubunge Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini
Social Plugin