Mshindi wa Kura za maoni tarafa ya mjini Shella Mshandete(Kushoto) na Zuhura Waziri (Kulia) Mshindi wa kura za Maoni Udiwani viti maalum Tarafa ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga wakifurahia baada ya ushindi wao.
Na Shinyanga Press Club Blog
Na Shinyanga Press Club Blog
Mchakato wa Kuwapata Madiwani wa viti Maalum ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM umefanyika leo nchini ambapo mkoani Shinyanga pia zoezi hilo limefanyika na Jimbo la Shinyanga mjini limekamilisha zoezi hilo kwa kuwapigia kura za maoni Wagombea 29 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo
Akitangaza Matokeo ya kura hizo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Jasinta Mboneko amesema kuwa kura hizo si ushindi bali ni mchakato wa mwanzo kuelekea kuwapata watakaopeperusha bendera ya chama hicho.
Ambapo Tarafa ya Mjini iliyokuwa na Wagombea 20 washindi waliopatikana ni Kanji Moshi aliyepata kura 152, Seni Paschazia amepata kura 112, Ester Makune amepata kura 108 na Shella Mshandete amepata kura 103.
Huku Pika Shongole kutoka Tarafa ya Old Shinyanga akiibuka na ushindi wa Kura 111 dhidi ya wapinzani wake wawili na Zuhura Waziri akiibuka Mshindi toka Tarafa ya Ibadakuli aliyepata kura 162 dhidi ya wapinzani wake wawili.
Huku Pika Shongole kutoka Tarafa ya Old Shinyanga akiibuka na ushindi wa Kura 111 dhidi ya wapinzani wake wawili na Zuhura Waziri akiibuka Mshindi toka Tarafa ya Ibadakuli aliyepata kura 162 dhidi ya wapinzani wake wawili.
Mboneko amesema kuwa jumla ya Wajumbe 192 wamepiga kura kati ya 198 waliopaswa kuhudhuria na kubainisha kuwa jumla ya tarafa tatu zimeshiriki katika uchaguzi huo ambazo ni Old Shinyanga ambapo wamejitokeza wagombea watatu ambao ni Nyasamba Mussa aliyepata kura tatu, Swedi Abdul kura 84 na Chongole Pika kura 111.
Aidha katika tarafa ya Ibadakuli waliogombea ni watu watatu ambao ni Kawani Mdaki aliyepata kura 12, Regina Enock kura 34 na Zuhura Waziri kura 162.
Kwa upande wa Tarafa ya mjini wagombea 20 wa tarafa ya mjini wamejitokeza kati yao washindi wanne wa kura za Juu ndiyo wamepitishwa kuwa washindi akiwemo Seni Paschazia aliyepata kura 112, Ester Makune kura 108, Shella Mshandete kura 103 na Kanji Moshi kura 152.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Shumbuo Katambi amewataka wajumbe kuacha makundi yaliyokuwepo badala yake washikamane ili kuleta ushindi wa chama cha mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu.
Shambuo ameongeza kuwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanapaswa kuhakikisha wanasimama imara katika kuleta ushindi wa CCM unaotarajiwa kufanyika Octoba 28 Mwaka huu
Naye mmoja wa Wagombea aliyeshinda kura hizo za maoni Bi Zuhura Waziri amesema kuwa kurejea kwake kwa mara ya pili baada ya kupitishwa na wajumbe wa chama hicho ni ishara ya utendaji kazi bora kwa wanachama na wananchi wa tarafa ya Ibadakuli hivyo ataitumia fursa hiyo kwa mara nyingine kwenda kusukuma gurudumu la maendeleo katika tarafa yake.
Baadhi ya Wagombea wa Udiwani Viti Maalum Manispaa ya Shinyanga wakiwa wameketi wakiendelea kusubiri mchakato wa Upigaji Kura za Maoni.
Wajumbe wakisubiri kutekeleza wajibu wao wa kuwapigia kura wagombea
Katikati ni Mgombea wa Nafasi ya udiwani Viti maalum toka Tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri akiwatazama wajumbe
Msimamizi wa Uchaguzi wa viti Maalum udiwani jimbo la Shinyanga Mjini ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisisitiza jambo kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji wa kura za maoni.
Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya udiwani akiwaomba wajumbe kumpigia kura ili aweze kuwasilisha kero zao katika baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga akiwa amepiga Magoti kwa unyenyekevu.
Mgombea akionyesha namba yake ya kupigiwa kura huku wajumbe wakisubiri kufanya yao na kupigia kura wanayeona ametoa sera za kuridhisha
Mgombea akiendelea kujinadi na kubainisha sera zake kwa wajumbe
Miza Jilala Mgombea nafasi ya udiwani tarafa ya Mjini Akiomba kura kwa wajumbe huku akionyesha unyenyekevu ya kuwa licha ya umri mdogo lakini ana uwezo wa kuwatumikia wanawake wa Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa Wagombea ambaye ni mlemavu akiomba kupewa ridhaa ya kuwakilisha katika baraza la manispaa ya Shinyanga Mjini kupitia Kura za Wajumbe.
Suzany Butondo mgombea wa Udiwani viti Maalum tarafa ya Mjini akiomba kura kwa wapiga kura huku akiinamisha kichwa chini ishara ya kuwaangukia wajumbe wamfanyie wepesi katika kumpigia kura za maoni ambaye amebainisha kutatua kero zao.
Wagombea wa Nafasi ya Udiwani Viti Maalum Tarafa ya Ibadakuli Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wakiwa wameketi pamoja na kuwashukuru wajumbe.
Msimamizi akiwaambia jambo wajumbe na washindi wote baada ya kuhitimisha zoezi la kupiga kura za maoni
Washindi wa Kura za maoni wakifurahia kupitishwa na wajumbe
Zuhura Waziri akikumbatiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza Muda wake Salome Makamba
Washindi wa Kura za Maoni Udiwani Viti Maalum Jimbo la Shinyanga mjini Wakiwa katika Picha ya Pamoja
Wagombea wakiendelea na Zoezi la kupiga Magoti
Mgombea aliyeshindwa kufikisha kura akiwashukuru wajumbe na wapiga kura
Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Shambuo Katambi akiwashukuru wajumbe na wanachama wote kwa kuhitimisha zoezi katika mazingira salama
Social Plugin