Vijana wa Chama Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni wamemchukulia fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.
Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, Suleiman Masauni amewataka wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais kujitokeza na kuchukua fomu ambazo gharama yake ni shilingi laki 5.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Ilala, Salim Muslim amesema jumuiya ya vijana imefikia uamuzi huo baada ya kutafakari na kuona kiongozi huyo anazo sifa za kugombea nafasi Urais kutokana na ubobezi katika masuala ya uchumi.
Tayari tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza tarehe ya kuanza kampeni ambayo ni Agosti 26 na uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Social Plugin