Wakili Hassan Athuman Fatiu maarufu 'Mtoto wa Muuza Kahawa' akionesha fomu ya Kuomba Kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Hassan Athuman Fatiu ambaye ni Wakili na Mkulima wa mpunga, mkazi wa kata ya Kitangili amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga kipaumbele chake kikubwa ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM na vipaumbele binafsi vitakavyofikishwa katika ofisi ya mbunge. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin