MgombeaUbunge viti maalumu Suzana Senso kupitia CCM akirudisha fomu kwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tarime Sauda Kashombo (kulia)
Na Dinna Maningo - Malunde1 blog Tarime
Wanawake kumi na mbili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime wamechukua na kurudisha fomu za kuomba kugombea nafasi za Ubunge uwakilishi na viti maalumu na kwa Udiwani viti maalumu wakiwa 63.
Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tarime Sauda Kashombo aliwataja wagombea hao kuwa ni Patricia Rhob Kabaka kundi la Viti maalumu wanawake,Bitrice Raya Kundi la wasomi,Getruda Emanuel kundi la wanawake,Beatrice Kebaso kundi la Wafanyakazi,Mosi Magere kundi la Wanawake,Rosemary Masirori kundi la Walemavu .
Wengine ni Suzana Senso Kesogwe kundi la wafanyakazi, Ghati Chomete,Nansi Msafiri,Salma Hamidu Musa na Bhoke John wote wakigombea kundi la wanawake.
Kashombo alisema kuwa nafasi ya Udiwani viti maalumu watia nia wako 63 ambapo Tarafa ya Ingwe ni 15,Inchage 28,Inano 10,na Inchugu 10.
Aliongeza kuwa katika nafasi ya Kata watia nia wanawake ni 6.