WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo kushoto akizindua Jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga leo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo katikati akitoka kwenye Jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga mara baada ya kulikagua kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo wa pili kutoka kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati alipotembelea mradi wa kitega uchumi cha stendi ya mabasi kange Jijini Tanga wakati wa ziara yake wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo
Ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi cha Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenye stendi ya Mabasi Kange Jijini Tanga mafundi wakiendelea na ujenzi
Muonekano wa Jengo jipya la Halmashauri ya Jiji la Tanga
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo ametaka dampo la kisasa la Mpirani Jijini Tanga lilindwe kwa sababu ni uchumi na limetumia kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wake mpaka lilipokamilika huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kwenda na viroba kuchukua kokoto.
Amesema kwani kokote hizo zimemwagwa kwenye dampo hilo kwa ajili ya kulinda dampo hilo ambalo litakuwa la kisasa kwa Jiji hilo tokea lilipoanzishwa huku akieleza ujenzi huo umetokana na mapenzi mwema ya serikali ya awamu ya tano Dkt John Magufuli kuwadumia watanzania.
Jafo aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake Jijini Tanga ambapo alitembelea mradi mbalimbali na kufanya uzinduzi ambayo ni ujenzi wa dampo la kisasa mpirani, ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Jiji hilo,Ujenzi wa mradi wa mkakati wa Jengo la kitega uchumi stendi ya mabasi
Baada ya kutembelea dampo hilo alionekana kuridhishwa na ujenzi wake huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na watendaji wake ikiwemo wasimamizi wa mradi huo kutoka Tarura Makao Makuu.
Sambamba na maeneo hayo lakini pia Waziri huyo alitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Kange stendi kuu ya mabasi ambapo kote alipopita alionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema katika maeneo mengine ya dampo wakati unapokwenda kutembelea unaona hofu ya kufika lakini kwenye dampo hilo tokea nimefika hapo sikikii harufu yoyote hivyo mkurugenzi na watendaji wake mmefanya kazi kubwa sana .
Waziri huyo alisema mradi huo umepata umepata mafanikio makubwa kwani Tanga ya mwaka 2015 sio ya mwaka 2020 hivyo dada zangu walikuwa na viatu vya mchuchumio na nywele wanaweza kutengeneza vizuri lakini wanashindwa kutembea lakini kwa sasa wanaweza kutembela bila kuwepo na hofu.
“Pongezi kwa Jiji la Tanga ujenzi wa hospitali ya wilaya eneo la Masiwani mmepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya leo nimepata taarifa huduma zinatolewa na Rais ametoa fedha nyengine za ujenzi wa vituo vyengine hapa Tanga maana yake wananchi waliokuwa wanatembela umbali mrefu sasa watapata huduma karibu tena vituo vilivyoboreshwea kwa kisasa”Alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo alisema kwamba watumishi wa halmashauri msingesimama pamoja kwa ajili ya miundombinu hiyo ambayo imejengwa kwa gharama ya milioni 400 mpaka milioni 500 wakati vituo hivyo kipindi cha nyuma vilikuwa vinajengwa kwa wastani wa bilioni 2 wakaelekeza vituo hivyo vijengwa kupitia fedha ya ndani (Force Acount).