WCF YATWAA TUZO YA MSHINDI WAKWANZA KUNDI LA TAASISI ZA BIMA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII MAONESHO YA 44 YA SABASABA



Waziri wa Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Sa;lum Ali (kushoto), akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, baada ya kuibuka mshindi wa muoneshaji bora kundi la Taasisi za bima na hifadhi ya jamii, katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele leo Julai 13, 2020 katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Bw. Mshomba akionyesha tuzo hiyo mbele ya banda la WCF viwanja vya Julius Nyerere, maarufu Sabasaba mara baada ya kukabidhiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba akiungana na wafanyakazi wa Mfuko waliokuwa wakihudumia wananachi waliotembeela banda hilo wakati wakisherehekea ushindi huo.
Bw. Mshomba katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko, wakiwa na tuzo hiyo.
Bw. Mshomba akiwashukuru wafanyakazi wake waliokuwa wakihudumia wananchi katika banda hilo kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kwa weledi.
***

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya muoneshaji bora kundi la Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba amepokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali wakati wa kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 13, 2020.

“Kusema kweli siku ya leo tunayo furaha sana mimi mwenyewe na wafanyakazi wenzangu wote, kwa mara ya kwanza tumeweza kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya bima na mifuko ya hifadhi ya jamii, hii inadhihirisha kwamba penye nia pana njia, mwaka jana tulikuwa washindi wapili tukaweka azma kwamba walau siku moja tuwe washindi wakwanza na leo imefika tunashukuru sana.” Alisema Bw. Mshomba na kuongeza….

Ushindi huu unaendana na vision ya Mfuko, tumejiwekea malengo ya kuwa taasisi ya kuigwa sio tu hapa Tanzania lakini Afrika hususan katika taasisi za hifadhi ya jamii na haswa katika Mifuko ya Fiadia na tunapokuwa wakwanza katika maonesho haya makubwa hapa nchini hiyo inaonyesha kwamba tumko katika njia sahihi na lengo letu ni kuendelea kushika nafasi kama hizi katika maonesho na shughuli mbalimbali tunazoshiriki.

“Huduma zetu ni bora tumeboresha sana huduma zetu na kwa sasa zinapatikana kupitia mtandao (online portal) na waliofika katika banda hili wameelezea jinsi walivyovutiwa na huduma zetu zote zinapatikana kupitia mtandao na ule usumbufu kwa wateja haupo kabisa kwa sababu Mafao yanalipwa kupitia mtandao, lakini hata taarifa za kutokea ajali au kuumia kazini zinawasilishwa kupitia mtandao, usajili wa waajiri na wanachama wenyewe ni kupitia mtandaoni, , kitu kwa sasa tunafanya kupitia mtandao, usajili wa waajiri ni kupitia mtandao, ukusanyaji wa michango ni kupitia mtandaoni kwahivyo kila kitu tunafanya kwa kutumia mtandao na hilo kwakweli limewezesha kuboreshwa kwa shughuli zetu na nia yetu kwakweli ni kuwa kileleni.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post