Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.
Akizungumza jana na mamia ya wafuasi wa chama hicho, katika eneo la Njia Nne, wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Zitto alisema, anamkaribisha Membe ndani ya ACT- Wazalendo kwa mikono miwili
“Tunamtaka Membe kujiunga na chama chetu, ili kuihami demokrasia na kupigania haki za wananchi,” alieleza Zitto na kuongeza, “mtu yoyote anayeona ukandamizaji haufai, anapaswa kuungana na wenzake, kupinga vitendo hivyo.
"Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala"
Social Plugin