Staa wa muziki nchini, Diamond Platnumz amemzawadia Zuchu gari mpya aina ya Toyota Vanguard hapo jana katika show ya Big Sunday Live ya Wasafi TV.
Zawadi hiyo imetolewa ndani ya saa 24 tangu Zuchu afanye show kubwa yenye mafanikio makubwa ndani ukumbi wa Mlimani City ya kuwashukuru mashabiki zake kwa mapokezi makubwa waliyompatia kwa kipindi kifupi alichokuwepo kwenye muziki.
Katika ujumbe ambao ameuchapishwa kwenye mtandao wake wa Instagram, amemuelezea Diamond kama Boss mwenye moyo wa kipekee sana.
"Mwenyezi Mungu wangu nasema Alhamdulillah,Mbariki boss wangu na umuongeze kwa hiki kikubwa alichoniongezea kwenye maisha yangu.
"Si kila mtu anamoyo kama wako boss Hakunaaa cha kukulipa My brother hakuna kwakweli Allah akupe umri wa uhai wenye mafanikio zaidi unatuokoa wengi sana Diamond Platnumz Asante boss. "-Zuchu
Ikumbukwe kuwa, Malkia huyo mpya wa kizazi kipya, officialzuchu amezawadia gari ikiwa ni miezi mitatu tu tangu ajiunge na lebo ya WCB ambayo inamilikiwa na Diamond.
Social Plugin