Joto la uchaguzi limezidi kupanda kwenye Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro,baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo hilo huku akisindikizwa na mamia ya wakazi wa eneo hilo, huku ajinasibu kutatua kero zilizodumu kwa muda mrefu kwenye Jimbo hilo ikiwemo tatizo la maji.
Jimbo la Rombo limekuwa chini ya Chadema kwa miaka 10,ambapo Prof. Mkenda amejinasibu kufanya siasa za Kisayansi kwa ajili ya Maendeleo ya wananchi wa Rombo na siyo Siasa za porojo.
Wanachama wa CCM wakisindikiza Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo la Rombo
Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo hilo akisaini kitabu baada ya kurejesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Rombo
Social Plugin