Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMRI KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA JIMBO LA KISHAPU


Katikati ni Iddi Salum Amri  kupitia Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) akiwa na wanachama wa CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Kishapu. 


Na Sumai Salum - Malunde 1 blog
Mgombea ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Iddi Salum Amri  kupitia Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Akizungumza Agosti 13,202 wakati wa kuchukua fomu kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Emmanuel Matinyi, Amri alidai kuwa anagombea ili aweze kuwawakilisha Wana Kishapu kwa kuwa wamekosa wawakilishi kwa muda mrefu ili kuwasaidia kuwaondolea changamoto wanazokutana nazo.

“Makusudio makubwa kama kijana msomi nimewiwa kugombea nafasi hii kwa kuwa Kishapu ina changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa barabara,maji pamoja na ajira kwa vijana na pia nashukuru chama changu cha CHADEMA kwa kuniamini na kunipa nafasi hii huku makusudio makubwa ni kuleta maendeleo katika jimbo hili”,alisema Amri.

Naye  msimamzizi wa uchaguzi ,Matinyi alisema kuwa uchaguzi mkuu unaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,sheria ya uchaguzi sura namba 343 na sheria wa uchaguzi serikali za mitaa sura namba 292 huku akizungumzia kanuni za maadili zinaz ongoza uchaguzi huo.

“Tume ya uchaguzi tumejipanga sawasawa kusimamia uchaguzi kuwa wa kweli,wazi na wa haki ila Jambo la msingi nataka niwaambie wagombea wafanye kampeni kwa amani bila uvunjifu wa amani na pia wahakikishe wanafuata kanuni za maadili na maelekezo mbalimbali ambayo tumetoa kupitia kwa wagombea wenyewe na pia katika vikao vya pamoja tunavyovifanya kati ya tume na vyama vya kisiasa”,alisema Matinyi.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kishapu, Elias Maico alisema kuwa Iddi Amri ameteuliwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho kupitia mkutano mkuu wa Agosti 6 mwaka huu na kupita kwa kura zote za ndiyo hivyo wanaamini atawakilisha vyema CHADEMA katika utendaji kazi wake kwa wananchi.




Mgombea ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Iddi Salum Amri kupitia Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) akikabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Emmanuel Matinyi (kulia).




Mgombea ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Iddi Salum Amri kupitia Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) akiwa na wanachama wa CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Kishapu.







Viongozi wa Chadema, wasimamizi wa uchaguzi pamoja na wajumbe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com