BRIGHTERMONDAY YATOA MWONGOZO KUSAIDIA WAAJIRI KUSIMAMIA RASILIMALI WATU WAKATI NA BAADA YA MAJANGA



BrighterMonday yazindua Kijitabu cha Mwongozo kwa Mwajiri (Employer Handbook) kinachoangazia namna bora za kufanya usimamizi wa rasilimali watu wakati wa majanga kama ya Corona na hata baada ya hapo.


Katika kijitabu hicho, pamoja na masuala mengine kinaangazia hatua muhimu katika mchakato wa uajiri na ufanyaji maamuzi, mazingira na namna ya kufanya kazi kutokea majumbani au bila kuwepo ofisini na sera za ufanyaji kazi kutokea nyumbani na zana za kuwezesha kufanikisha hilo.

Vilevile, Kijitabu cha Mwongozo kwa Mwajiri kimegusia masuala ya mawasiliano yenye ufanisi na wafanyakazi, Usimamizi wa Utendaji wa Wafanyakazi na Ustawi pamoja na mkakati wa rasilimali watu baada ya janga la corona

Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa kutumia mjumuisho wa mbinu ikiwamo taarifa zilizokusanywa kutoka kwenye tafiti za nje, wataalamu wa Rasilimali watu wa Brighter Monday na wataalamu wa rasilimali watu kutoka kwenye makampuni mbalimbali nchini Tanzania.

Kitabu hiki kinakusudia kuwasaidia wale waliopo kwenye sekta ya usimamizi wa rasilimali watu wakati wa majanga na  hata huko baadaye. Kinaweza kutumika kama mwongozo  kuweka dhana katika utendaji na kutengeneza mbinu zinazofaa zaidi katika eneo la kazi. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kijitabu hicho, Mkurugenzi wa BrighterMonday Tanzania Reshma Bharmal-Shariff “Sote tunafahamu kuwa tulipita katika changamoto ambayo hatukuitarajia lakini pia haikuwa kutoke kabla.
Hii ilitufanya sisi kama wadau wa rasilimali watu kuona haja kubwa ya kutoa ushauri na maoni ya wataalamu mbali mbali katika sekta ya rasilimali watu. 

Amesema kuwa kitabu hiki kinalenga kusaidia watendaji na wadau wa rasilimali watu kufahamu mbinu na taratibu sahihi za kuongoza na kusimamia timu kwa ufasaha zaidi wakati wanapopata changamoto na hata baada. Waaajiri na kuwasaidia waajiriwa kupata mwongozo wa kuboresha eneo la kazi. Vilevile, kitabu hiki kinawafaa hata wale wanaotafuta ajira kufahamu ni mchakato mzima wa uajiri. 

Vilevile Meneja Masoko wa BrighterMonday Tanzania, Erca Uisso alisema “Kijitabu hiki ni bure kwa kila mmoja na kinapatikana kwa mfumo wa nakala tepe inayopatikana kwenye tovuti ya Brighter Monday Tanzania BOFYA HAPA au kwa kutembelea kiungo hiki https://www.brightermonday.co.tz/research”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post