Na Suzy Luhende - Kishapu
Shangwe zimetawala wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakati Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Boniphace Nyangindu Butondo akikabidhiwa fomu ya kugombea Ubunge na msimamizi wa uchaguzi kutoka Tume ya uchaguzi Emmanuel Johnson katika ofisi ya halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Shangwe zimetawala wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakati Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Boniphace Nyangindu Butondo akikabidhiwa fomu ya kugombea Ubunge na msimamizi wa uchaguzi kutoka Tume ya uchaguzi Emmanuel Johnson katika ofisi ya halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Butondo amechukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Kishapu Jumamosi Agosti 22,2020 akisindikizwa na viongozi na wanachama wa CCM.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Boniphace Nyangindu Butondo amesema amefurahishwa na baadhi ya wagombea wenzake waliojitokeza katika uchaguzi wa kura za maoni kwa kuonyesha ushirikiano wa kumsindikiza kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia chama hicho akieleza kuwa wameonyesha moyo wa upendo na kuwaomba wawe na ushirikiano huo huo mpaka watakapochukua ushindi.
"Ninafuraha sana kuwaona hapa ndugu wagombea wenzangu katika kura za maoni kwa ajili ya kunisindikiza nikachukue fomu, mmeonyesha upendo wa dhati hivyo naombeni ushirikiano wenu, Katika uchaguzi huu ili tuweze kupata ushindi kwa asilimia 100, kwani hakuna kinachoshindikana yote yanawezekana kwa uweza wa Mungu",amesema Butondo.
"Ninawashukuru viongozi wa dini wote mliokuja na wale ambao hamjafanikiwa kuja,naomba muendelee kuniombea, na kumuombea Rais wetu na kuiombea nchi ya Tanzania iendelee kuwa na amani na upendo .Ninawashukuru wazee wangu wote mliofika hapa kwa ajili ya kunisindikiza ninaahidi kwamba nitashirikiana nanyi mpaka mwisho nitahitaji mawazo yenu na Mungu atatusaidia"amesema Butondo.
Baadhi ya wagombea/watia nia waliojitokeza kumsindikiza Butondo ni Sangalali Emmanuel, Kishiwa Frances, Boaz Mihulu, Dulla Daniel, Joseph Kwilasa, na Shagembe Mipawa ambao wameahidi kushirikiana naye kwa hali na mali ili kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu 2020.
"Tunaahidi kumuunga mkono mgombea wetu aliyeteuliwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi mpaka tuhakikishe anapata ushindi, tutakuwa naye bega kwa bega, tunakiomba Chama Cha Mapinduzi kitupe nafasi wakati wa kampeni tupo tayari kufanya kazi wakati wowote ili tupate ushindi",amesema Boaz Mihulu.
Naye Shagembe Mipawa amesema mgombea ubunge aliyeteuliwa ni mwenzao hivyo watahakikisha wanapigana mpaka mwisho ili kuhakikisha wanachukua ushindi mapema asubuhi kwa asilimia 100.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kishapu
Emmanuel Johnson amesema wanatakiwa kujenga imani ya kuaminiana waiamini tume ya uchaguzi na kuaminiana wao kwa wao ili waweze kufanya kitu kizuri na wawe na umoja na mshikamano.
"Sisi kama tume tumejipanga kuendesha uchaguzi huu kwa haki,kwani tunajua siasa ni upendo, hivyo tunakupa fomu nne ukazijaze vizuri kwa uangalifu uwe na wadhamini wasiopungua 25 wawe ni wadhamini waliojiandikisha na njia nzuri pateni wadhamini wengi jinsi mnavyoweza ili kama kuna mtu atabadilisha mawazo inabaki kolamu hiyo hiyo",amesema Msimamizi wa uchaguzi Johnson.
Pia amewaomba wakafuate sheria na utaratibu kama hataelewa sehemu afike katika ofisi ya msimamizi apate maelekezo kabla ya kurudisha fomu.
Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu ambaye ni katibu wa vijana wilaya hiyo Jamal Namangaya amesema wanaamini watakuwa wastaarabu zaidi hivyo wasimamizi wasiwe na mashaka kwani wao yuko vizuri anaweza kujieleza pia anampenda Mungu.
Mwenyekiti CCM wilaya Shija Ntelezu amesema kama walivyoshirikiana kuchukua fomu na wagombea wenzake wa kura za maoni na kwenye kurudisha fomu na kampeni aliomba uwepo ushirikiano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Kishapu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Boniphace Nyangindu Butondo akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge na msimamizi wa uchaguzi kutoka tume ya uchaguzi Emmanuel Johnson (kulia) katika ofisi ya halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga leo Jumamosi Agosti 22,2020. Picha na Suzy Luhende
Awali Boniphace Nyangindu Butondo akikabidhi barua ya uteuzi kutoka CCM kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kishapu, Emmanuel Johnson
Wanachama wakimsindikiza mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Boniphace Nyangindu Butondo kwenda kuchukua fomu katika halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga
Wanachama wakimsindikiza mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Boniphace Nyangindu Butondo kwenda kuchukua fomu katika halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga
Boniphace Nyangindu Butondo akiwa na baadhi ya wagombea/watia wenzake waliogombea katika kura za maoni waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu ambao wamesema watashirikiana nae ili ashinde kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu.
Vijana wa CCM Kishapu waliojitokeza kumsindikiza mgombea ubunge Boniphace Nyangindu Butondo kuchukua fomu ya kugombea ubunge
Vijana wa CCM Kishapu waliojitokeza kumsindikiza mgombea ubunge Boniphace Nyangindu Butondo kuchukua fomu ya kugombea ubunge
Boniphace Nyangindu Butondo akiwa na baadhi ya viongozi wa dini
Social Plugin