BENKI YA CRDB YACHANGIA MIFUKO YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI TINDE


Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akimkabidhi mifuko ya saruji, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba (mwenye nguo ya kijani) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo (wa pili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga leo Alhamis Agosti 6,2020. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney .Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akimkabidhi mifuko ya saruji Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba (mwenye nguo ya kijani) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo (wa pili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde. 
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akimkabidhi mifuko ya saruji Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba (mwenye nguo ya kijani) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo (wa pili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde.
Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tinde, Agnes Mnyipembe wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba (mwenye nguo ya kijani) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo. 
Muonekano wa mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kupitia tawi la Tinde na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 
Muonekano wa mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kupitia tawi la Tinde na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 
Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la Kituo cha Polisi Tinde. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba akielezea kuhusu ujenzi wa jengo la kituo cha polisi Tinde lenye huduma zote muhimu unaotarajia kugharimu takribani shilingi milioni 80. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba (katikati) akiwaonesha maafisa kutoka Benki ya CRDB na Wajumbe wa Kamati ya ujenzi mchanga kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo cha polisi Tinde. 
Maafisa kutoka Benki ya CRDB na Wajumbe wa Kamati ya ujenzi jengo la kituo cha polisi Tinde wakiangalia karo la maji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo cha polisi Tinde.


**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imetoa msaada wa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Jengo la Kisasa la Kituo cha Polisi Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mifuko hiyo imekabidhiwa leo Alhamis Agosti 6,2020 na Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo.

Akikabidhi mifuko ya saruji, Wagana alisema mchango huo wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo cha polisi Tinde, ni sehemu ya utamaduni wa Benki ya CRDB kushirikiana na jamii inayowazunguka ili jamii ione umuhimu wa kuwa na Benki ya CRDB.

"Jeshi la polisi ni wadau wetu wazuri sana,ni wadau ambao wanatushika bega kikamilifu kuhakikisha kuwa Benki ya CRDB ina ulinzi wa kutosha kwa hiyo kama mdau wetu kwa upande wa ulinzi tumeona Benki ya CRDB kupitia tawi letu la Tinde tuchangie mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi",alisema Wagana.

 "Tumeanza kwa kuchangia mifuko ya saruji 30 katika hatua ya kwanza na tutaendelea kuwashika mkono. Bahati nzuri akaunti ya mradi huu wa ujenzi ipo katika Benki ya CRDB hivyo tutaona mwenendo wa michango ya wadau",aliongeza Wagana.

Aidha alisema Benki ya CRDB ni mdau wa maendeleo nchini Tanzania, na Benki inayoongoza kwa kusaidia jamii. 

"Jamii inatupa biashara hivyo kile kidogo tunachopata kwenye faida yetu tunakitoa kuonesha ushirikiano na mchango wetu kwa jamii lengo ni kuifanya jamii inayotuzunguka ione umuhimu wa Benki ya CRDB na kuendeleza ushirikiano zaidi na wadau wanaotuzunguka",alisema Wagana.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga,

Luther Mneney alisema ili maendeleo ya Tinde yaweze kuonekana na kuwa mahali salama pa kuwekeza ni lazima suala la ulinzi liimarishwe na ndiyo maana benki ya CRDB imeona umuhimu kwa kuchangia katika ujenzi wa kituo cha polisi.

Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde, Inspekta Richard Kapongo ambaye pia amechangia mifuko 30 ya saruji aliishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wa mifuko ya saruji na kueleza kuwa itasaidia kuongeza nguvu katika ujenzi wa jengo la kisasa la kituo cha polisi Tinde kinachojengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa maendeleo.

“Tunaishukuru Benki ya CRDB kwa kutuchangia mifuko 30 ya saruji yenye thamani ya shilingi 540,000/= na mimi nimechangia mifuko 30 ya saruji na leo tuna mifuko 60 ya saruji yenye thamani ya shilingi 1,080,000/=",alisema Inspekta Kapongo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la kituo cha Polisi Tinde, Juma Waryoba alisema ujenzi wa jengo la kituo cha polisi lenye huduma zote muhimu unatarajia kugharimu takribani shilingi milioni 80.

Alisema wameshaanza michakato ya ujenzi ambapo tayari wamejenga karo la maji,wamesafisha eneo la ujenzi,wamesomba mchanga na zoezi la kufyatua matofali linaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post