Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye ni Mgombea Urais Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA itashirikiana na vyama vingine vya siasa nchini Tanzania katika uchaguzi Mkuu 2020.
Tundu Lissu ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
"Tuko pamoja na tutakuwa pamoja,kila mtu amezungumza habari za ushirikiano na nakubaliana na wote waliotaka ushirikiano, tutashirikiana",amesem Lissu.
Naye Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Salum Mwalimu ambaye amechaguliwa na chama chake kuwa mgombea Mwenza Urais Tanzania kupitia CHADEMA pia amesema chama hicho kitashirikiana na vyama vingine vya siasa kwenye uchaguzi mkuu 2020.
"Tutakwenda Kushirikiana siyo kuungana kama wengine wanavyosema. Sisi Chadema bega moja lipo ACT Wazalendo,bega jingine lipo CHADEMA tupo tayari kwa ushirikiano.Kazi imeanza na nafikiri tutaimaliza salama",amesema Mwalimu.
Social Plugin