Mgombea Ubunge Jimbo la Msalala, Iddi Kasimu akipokea fomu ya uteuzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Msalala Simon Berege. Picha zote na Salvatory Ntandu - Kahama
Mgombea Ubunge wa jimbo la Ushetu, Elias Kwandikwa (aliyevaa shati la njano) akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM baada ya kukabidhiwa fomu za uteuzi wa Jimbo la Ushetu leo Agosti 21, 2020.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Ushetu Eliasi Kwandikwa (kushoto) akipokea fomu ya Uteuzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ushetu, Michael Matomora.
Mgombea Ubunge Jimbo la Msalala, Iddi Kassim akiwasilisha barua ya Uteuzi ya kugombea Ubunge kutoka katika chama chake (CCM) kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Msalala Simon Berege.
Baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Kahama wakiwa katika ofisi za Mkurugezi wa Uchaguzi Jimbo la Msalala.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emanuel Mbamange akimwongoza mgombea ubunge jimbo la Ushetu, Elias Kwandikwa kungia katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi jimbo la Ushetu.
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Wagombea Ubunge walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika majimbo ya Msalala na Ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, leo wamechukua fomu katika ofisi za wakurugenzi wa uchaguzi kwa ajili ya maandalizi ya kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Mapema leo Mgombea Ubunge Jimbo la Msalala kupitia (CCM) Iddi Kassimu Iddi amefika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Msalala, Simon Berege na kukadhiwa fomu akiambatana na viongozi wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Thomas Myunga na Katibu wa chama hicho wilaya ya Kahama, Emanuel Mbamange na viongozi wengine kwaajili maandalizi ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Baada ya kukabidhiwa fomu hizo Iddi amewashukuru wanachama na viongozi wa chama hicho kwa kumpa ridhaa ya kugombea jimbo hilo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wote wa jimbo hilo pindi atakapo chaguliwa kuwa kuliongoza jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Katika Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alifika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Michael Matomora na kukabidhiwa fomu za kugombea ubunge katika jimbo hilo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya, Thomas Myonga.
Kwandikwa ambaye pia ni Naibu waziri wa uchukuzi, amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa awamu nya pili atahakikisha anawaunganisha wananchi wote kwa kihakikisha anatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani za maji, afya, elimu na miundombinu ya barabara.
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emmanuel Mbamanga amesema kuwa atahakikisha wagombea wote wa ngazi za udiwani na ubunge katika majimbo ya Msalala, Ushetu na Msalala wanapata ushindi katika Uchaguzi mkuu ujao.
“Kwa sasa wagombea wetu wanaendelea kuchukua fomu za tume ya Taifa (NEC) katika nafasi mbalimbali walizoziomba,” amesema Mbamange.
Social Plugin