Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
******
Na Majid Abdulkarim, Dodoma
Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hivi karibuni watanzania wataanza kuona faida kupitia mavuno ya miradi waliyoanza kutekeleza ndani ya miaka mitano ambayo ni Mavuno ya reli ya SGR, Umeme wa Bwawa la Nyerere, barabara mbalimbali, ujenzi wa Meli katika maziwa mbalimbali.
Aidha Dkt. Magufuli ameaidi watanzania kuwa wakimrudisha madarakani kazi yake ya kwanza atakayoifanya ni kujenga uwanja mkubwa wa michezo katika Jiji la Dodoma.
Dkt. Magufuli amebainisha hayo katika Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kitaifa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Dkt. Magufuli ameeleza kuwa Kazi alizofanya ndani ya miaka mitano ndizo zimewafanya kurudi kuomba tena ridhaa ili waweziendeleze zisije kukwama, wamenunua Ndege mpya 11, nane zimefika na tatu zinatengenezwa, katika Ilani mpya ya Uchaguzi amesema watanunua Ndege nyingine tano mpya ndani ya miaka 5 ikiwemo ya mizigo.
“Mkituchagua tumepanga kununua ndege nyingine tano, mbili za masafa ya mbali, mbili masafa ya kati na moja ya mizigo hivyo Tupeni kura za ndio tukakamilishe haya yote” amessema Magufuli.
“Mwaka 2015 Watanzania walitaka mabadiliko na Serikali ya awamu ya 5 imejitahidi kukata kiu zao, tumerudisha nidhamu Serikalini sasa hivi maofisini mnahudumiwa vizuri,tumedhibiti rushwa na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na waliofikishwa Mahakamani sio dagaa ni samaki wakubwa”ameeleza Dkt. Magufuli.
“Tutahamasisha pia wataalamu wetu wanaoweza kutibu magonjwa kwa kutumia dawa za kienyeji ili watambuliwe kikamilifu badala ya kuwapuuza, tutaongeza fedha kwa ajili ya utafiti na kusomesha Watanzania kwenye Vyuo bora” amesisitiza Dkt. Magufuli
Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli amesema kuwa wamepanga kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia Mil 5 2025, na mapato kutoka Dola Bil 2.6 hadi Dola Bil 6, kupanua wigo wa vivutio vya Utalii, ikiwemo kukuza Utalii wa mikutano na uwindaji wa Wanyamapori na kuimarisha utalii wa fukwe.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kuliongoza na kulisimamia taifa ili hatimaye kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa amani na usalama na huku watanzania kubaki wamoja.
” 2015 Watanzania walitaka mabadiliko ya kuona vitendo vya rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma unakomeshwa na walitaka mabadiliko ya kuona rasilimali za nchi zinalindwa na walitaka mabadiliko ya uchumi wa nchi ukue kwa kasi”, ameongeza Dkt . Maguful.
Pia Dkt. Magufuli amesema kuwa Watu wengi wanadhani yeye kutosafiri sana nje ya nchi basi uhusiano wa kidiplomasia umepungua, kitu ambacho si kweli na badala yake umeongezeka zaid , Balozi nane za Tanzania katika nchi 8 zimefunguliwa na mataifa mawili yamefungua Balozi zao mbili hapa nchini .
Lakini pia Dkt. Magufuli ameeleza kuwa mradi mkubwa wa FAR jijini Dodoma unatekelezwa , mradi huu utatatua changamoto ya upatikanaji wa maji Dodoma .
“Hadi sasa vijiji 9570 nchini vimeunganishwa na huduma ya umeme kutoka vijiji 2018 mwaka 2015, na hii ni kutokana na serikali kupunguza gharama ya kuunganisha umeme kutoka Sh. 177,000 hadi kufikia shilingi elfu 27 tu ” ameweka wazi Dkt. Magufuli
Hata hivyo Kuhusu usafiri wa anga tumekamilisha ujenzi wa Jengo jipya la Terminal 3, kule Dar es Salaam. Kwa hapa Dodoma tumepanga kujenga uwanja mkubwa ndege eneo la Msalato, uwanja huo utakua na Kilomita 3, hapa ndio makao makuu ya Nchi, kutakua na Ndege zinazoruka kutoka hapa Kwenda Ulaya”amesema Dkt. Magufuli
Kwa upande wake Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Mhe. Samia Suluhu ameeleza kuwa Katika miaka mitano wameweza kutekeleza kwa kishindo na wanaweza .
Huku Mgombea urais CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi amesema kuwa atafanya kazi na kuendeleza pale alipoishia Rais Ally Mohamed Shein. Nitakwenda kwa ‘speed”.
“Natoa wito kwa watanzania wote kulinda amani kwani bila amani hakuna maendeleo , hivyo tulinde amani yetu watanzania”, ametoa wito Dkt. Mwinyi
Katibu Mkuu CCM, Ally Bashiru amesema Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 inakurasa zaidi ya 300 Ikieleza Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka tano iliyopita na Uelekeo wa Miaka tano ijayo.
“CCM tunayo majimbo 18 kibindoni wagombea wetu wamepita bila kupingwa na sasa wanasubiri kuapishwa tu. Pia, tunazo kata zaidi ya 400 ambapo wagombea wetu wamepita bila kupingwa, mitambo imewashawashwa, moto uliowashwa atakayebabuka tusilaumiane,” ameeleza Dkt. Bashiru
Dkt. Bashiru ameendelea kusema kuwa Miaka mitano ijayo, CCM itaendeleza kuhimiza wananchi kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na maarifa kama msingi imara wa maendeleo ya taifa .
“CCM inatambua kuwa nchi yetu ina watu wenye uwezo na rasilimali za kutosha kama vile ardhi, madini, gesi asilia,misitu, wanyama, malikale, bahari, maziwa na mito” amesema Dk. Bashiru .
“CCM itaendelea kulinda na kuimarisha umoja, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama, kulinda, kuimarisha, kudumisha uhuru, Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na muungano wa Tanzania”, Dk. Bashiru
“Ndugu zangu wana Dodoma tunayo kila sababu ya kumchagua Magufuli kampeni yetu ya safari hii kwa sababu Madiwani wengi wamepita bila kupingwa na baadhi ya majimbo Wabunge wamepita moja kwa moja iwe ya Rais tu na iwe ya Nyumba kwa Nyumba” amesisitiza Spika Ndugai
Spika Ndugai ameeleza kuwa wengine lazima awape ripoti kazi yao ni kuzira, kununa na kutoka nje Bungeni,hivyo hadhani kama wananchi wanachagua watu kwenda Bungeni au kutoka, badala ya kuwa mali ya wananchi wanakuwa mali ya hivyo vyama.
Ikumbukwe Dkt. Magufuli anasimama jukwani kupeperusha Bendera ya CCM kwa mara ya Pili, ambapo Mara ya Kwanza ilikuwa ni Mwaka 2015.
Mgombea Mwenza kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mgombea Urai wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge Mteule kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Mh George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
Mbunge Mteule wa jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde naye akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni.
Mbunge Mteule wa jimbo la Kongwa Mh. Job Ndugai naye amezungumza machache katika mkutano huo
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa wamenyanyua mikono yao juu na Wananchi wa Dodoma hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Picha mbalimbali zikionesha umati wa wananchi wa jiji la Dodoma na viunga vyake walivyojitokeza kwa wingi ili kumsikiliza mgombea kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza na Wanamuziki wa Bendi ya TOT mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza na wasanii wa bendi ya TOT wakati alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumsalimia Rais wa Zanzibar na Makamo Mwenyekiti wa CCM alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba na viongozi mbalimbali hawapo pichani alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuuwa CCM Dk. Bashiru Ali katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanjwa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kushoto katika uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafuMh. Fredrick Sumaye.
viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mzee Philip Mangula akiwasili uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa ameketi jukwaani kulia ni Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa na Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Ali Idd.
(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DODOMA)
Social Plugin