Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele (kushoto) akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi (katikati) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Abubakari Gulam mara baada ya Patrobas Katambi kurudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumanne Agosti 25,2020.

Mgombea Ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi leo Jumanne Agosti 25,2020 amerudisha fomu ya kuomba kugombea ubunge kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi huku aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo,Stephen Masele akimuahidi kushirikiana naye bega kwa bega katika kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi.
Katambi ambaye aliambatana na viongozi na wanachama wa CCM akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ameahidi kufanya kampeni kwa amani na utulivu.
Mbunge mstaafu wa jimbo la Shinyanga mjini, Stephen Masele ameahidi kupigana kufa na kupona kuhakikisha CCM inashinda ngazi zote za udiwani, ubunge na Rais katika jimbo la Shinyanga mjini.
Aidha Masele amewataka WanaCCM kuungana na kuwaomba kuvunja makundi yaliyokuwepo na badala yake kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na chama huku akisisitiza kuwa atakuwa bega kwa bega na Katambi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu 2020.
Mgombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi akirudisha fomu kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi leo Jumanne Agosti 25,2020.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele (kulia) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Abubakari Gulam (katikati) wakiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi wakati akirudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Viongozi na wanachama wa CCM wakimsindikiza Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi kurudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini.

Social Plugin