Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Michael Kembaki akionyesha fomu na vitabu baada ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Tarime mjini
Na Dinna Maningo,Tarime.
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Michael Kembaki amesema kuwa atahakikisha anapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu 2020.
Akizungumza katika viunga vya ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tarime mjini mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge, Kembaki ambaye aliwahi kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi wa 2015 lakini kura hazikutosha na hivyo jimbo hilo kuongozwa na Esther Matiko kutoka Chama cha upinzani cha CHADEMA,amesema kwa sasa amejipanga vizuri na hatalipoteza jimbo.
"Nawashukuru wana CCM kwa kuniamini,namshukuru Rais wetu na kamati kuu kwakuniamini na kuniteua nawaahidi kwa vitendo nitasimamia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi,nitahakikisha tunapata ushindi wa kishindo hatutawaangusha wana CCM na kamati kuu ambayo walifanya maamuzi ya busara", alisema Kembaki.
Kembaki aliwaomba wana CCM Tarime na wananchi kumuunga mkono ili kuleta maendeleo ya kweli katika jimbo la Tarime mjini.
Baada ya mazungumzo hayo Kembaki akawatembelea na kuwasalimu wafanyabiashara wa maduka,wauza viazi ndani ya stend kuu ya mabasi na soko kuu ambapo akina mama wauza ndizi mbichi walimweleza wanavyosumbuliwa na kukamatwa.
"Wanawake tunaofanya biashara ya kuwauzia ndizi wasafiri tunapata shida tunafukuzwa kama Mbwa gari linakuja linabeba ndizi zetu kwamba hatutakiwi kufanya biashara stendi nawakati tuna vitambulisho vya wajasiliamali,Mimi namtoto niliyemwokota namlea mwenyewe sisaidiwi na mtu sina mwanaume hizi ndizi ndiyo zinanisaidia wanawake tunapata shida",alisema Mariam.
Kembaki aliwaahidi kuwa endapo akipata Ubunge atahakikisha anatatua kero za wafanyabiashara wakiwemo wanawake ambao wanasumbuliwa katika biashara zao.
Akiwa katika pitapita ya kuwasalimu wafanyabiashara zikasikika sauti za wanawake wauza matunda zikisema;
"Kwa kweli tuliposikia jina lako limerudi tumefurahi sana sisi wanawake ,Kembaki licha ya kushindwa Ubunge hakukata tamaa kutusaidia amefanya maendeleo mengi,safari hii huyu ndiyo tutampa kura.....Kembaki safari ile kura yangu ilipotea ila kwa sasa haitapotea lazima ushinde......"
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Michael Kembaki akionyesha fomu na vitabu baada ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Tarime mjini
Mama lishe akifurahia baada ya kusalimiwa na mgombea Ubunge Tarime Mjini, Michael Kembaki alipowatembelea wafanyabiashara kwenye kituo cha mabasi
Michael Kembaki akizungumza na wauza viazi stendi kuu ya mabasi
Michael Kembaki akizungumza na wauza viazi stendi kuu ya mabasi
Muuza ndizi na viazi stendi akionesha kitambulisho ambapo alimweleza Mgombea Ubunge Michael Kembaki kuwa wananyanyaswa na kukamatiwa ndizi licha ya kuwa na vitambulisho vya wajasiriamali.
Social Plugin