Wakili wa LHRC, Neema Jaji (Adv.) akizungumza katika mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu sheria na haki za binadamu kwa kuzingatia makundi maalum namna ya waandishi wa habari kwa usalama kazini, uandishi wa habari za uchunguzi unaozingatia takwimu na maadili ya uandishi wa habari. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Na Damian Masyenene - Geita
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita kuhusu sheria na haki za binadamu kwa kuzingatia makundi maalum namna ya waandishi wa habari kujikinga (usalama) wawapo kazini, uandishi wa habari za uchunguzi unaozingatia takwimu na maadili ya uandishi wa habari.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza Jumanne ya Agosti 18, 2020 na kuhitimishwa leo Agosti 20, 2020 yamefanyika mkoani Geita, yakilenga kuwaongezea ufahamu waandishi wa habari juu ya haki za binadamu, makundi maalumu, kufanya habari za uchunguzi na kujiepusha na hatari wawapo kazini.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius aliwahimiza waandishi wa habari kuzielewa haki za binadamu, kufanya kazi kwa weledi, huku akipendekeza Watanzania kushirikishwa zaidi wakati wa uandaaji wa sheria na kanuni mbalimbali ili kuzifanya haki za binadamu kuwa moja kati ya msingi wa katiba na kupewa ulinzi wa kutosha.
Naye Wakili wa LHRC, Neema Jaji (Adv.) aliwaomba waandishi wa habari kufanya kazi kwa mipaka yao kisheria na kuheshimu sheria za nchi na tamaduni zilizopo huku akisisitiza umuhimu wa kulinda makundi maalumu wakiwemo wanawake,watoto na watu wenye ulemavu,wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Akitoa mafunzo ya namna ya kufanya uandishi wa kiuchunguzi na kujilinda, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Peter Mataba aliwahimiza waandishi wa habari kufanya habari za uchunguzi ili kuisaidia jamii kujua yale yanayoendelea na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa, huku akiwataka kujali zaidi usalama wao kwani maisha yao ni muhimu zaidi.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Wakili wa LHRC, Neema Jaji (Adv.) akizungumza katika mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu sheria na haki za binadamu kwa kuzingatia makundi maalum namna ya waandishi wa habari kwa usalama kazini, uandishi wa habari za uchunguzi unaozingatia takwimu na maadili ya uandishi wa habari. Picha na Kadama Malunde,Vanny Charles,Joel Maduka na Baraka Abubakari
Wakili wa LHRC, Neema Jaji (Adv.) akizungumza ukumbini.
Wakili wa LHRC, Neema Jaji (Adv.) akiwahamasisha waandishi wa habari kuzingatia sheria na maadili ya uandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Peter Mataba akitoa mada kuhusu namna ya waandishi wa habari kujikinga wawapo kazini leo Alhamis Agosti 20,2020 wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Peter Mataba akitoa mada kuhusu uandishi wa habari za uchunguzi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Peter Mataba akiendelea kutoa mada ukumbini.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Peter Mataba akiendelea kutoa mada ukumbini.
Wawezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius (kulia) na Neema Jaji wakiwa kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita kuhusu sheria na haki za binadamu, namna ya waandishi wa habari kujikinga (usalama) wawapo kazini, kufanya kazi na makundi maalum na habari za uchunguzi.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akizungumza katika mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu sheria na haki za binadamu kwa kuzingatia makundi maalum namna ya waandishi wa habari kwa usalama kazini, uandishi wa habari za uchunguzi unaozingatia takwimu na maadili ya uandishi wa habari.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akizungumza ukumbini.

Waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.
Mafunzo yakiendelea
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo,Peter Saramba akizungumza wakati wa kufunga mafunzo.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo,Peter Saramba akizungumza wakati wa kufunga mafunzo.
Picha ya pamoja : Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita na wawezeshaji wa mafunzo kuhusu sheria na haki za binadamu, namna ya waandishi wa habari kujikinga (usalama) wawapo kazini, kufanya kazi na makundi maalum na habari za uchunguzi.

Picha na Kadama Malunde,Vanny Charles,Joel Maduka na Baraka Abubakari
Picha na Kadama Malunde,Vanny Charles,Joel Maduka na Baraka Abubakari
Social Plugin