Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na mgombea mwenza, Hamida Abdallah Huweishi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.
Profesa Lipumba ni mgombea wa saba kuteuliwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.
Pia, Philip John Fumbo wa chama cha DP ameteuliwa na NEC kugombea urais kwenye uchaguzi huo. Fumbo na mgombea wake mwenza, Zainabu Juma Khamisi wamekuwa wagombea wa nane kuteuliwa.
Vyama vilivyojitosa kuchukua fomu vilikuwa 17 kati ya 19 vilivyochukua fomu. Vyama ambavyo havikuchukua fomu kwenye nafasi hiyo ni TLP na UDP ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli.
Shughuli ya urejeshaji fomu itahitimishwa saa 10 jioni.
Social Plugin