Muonekano wa Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga lililozinduliwa leo Ijumaa Agosti 7,2020 na Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma.
****
Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, ambalo lilijengwa mwaka 2006 na kukamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi bilioni 4 limezinduliwa leo Ijumaa Agosti 7,2020 na Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma.
Akizungumza wakati wa kuzindua Jengo hilo, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma amesema lengo la kujengwa kwa jengo hilo ni kusogeza huduma kuwa karibu na wananchi.
Katikati ni Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma akikata utepe akizindua rasmi Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.