Mgombea urais nchini Tanzania kupitia Chama Cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele, amesema iwapo wananchi watakipa ridhaa chama chake kushika madaraka, serikali yake itatunga sheria ambayo makahaba, wasagaji na mashoga watakuwa wanachapwa viboko 200 na kwenda jela miezi sita.
"Mwili wa mtu si wa kufanyia biashara kingono, makahaba, wasagaji na mashoga wanaitia aibu nchi. Naomba wananchi wanikabidhi nchi nitawanyoosha," amesema Mwaijojele.
Amesema suala la rushwa limekuwa tatizo sugu nchini, hivyo serikali yake itahakikisha linashughulikiwa ipasavyo ili liishe kabisa.
Amesema mafisadi, watakatishaji fedha na wanaotorosha fedha nje watapewa adhabu ya kwenda jela miaka 50 na kupigwa viboko 200 baada ya kuhukumiwa.
Social Plugin