Stephen Julius Masele
Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Julius Masele ameaga rasmi Bunge la Afrika (Pan- African Parliament - PAP) baada ya muda wake kutumikia Bunge la Afrika kufikia kikomo.
Katika ujumbe wake wa kuaga Wabunge,wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Bunge la Afrika,Masele ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (2010-2020) amesema Mhula wa Bunge la Afrika na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinaenda sanjari hivyo nafasi yake imefikia tamati baada ya muda wake wa Ubunge nchini kufikia tamati.
“Mhula wa Bunge la Afrika unaenda samba na mhula wa Bunge la Tanzania.Baada ya kipindi cha ubunge kuisha ambacho kinaenda na uhai wa bunge la Afrika.Nafasi yangu ya Ubunge wa Afrika pia imefikia Tamati.
Kukosa nafasi ya kugombea Ubunge kunahitimisha rasmi nafasi yangu katika Bunge la Afrika”,amesema Masele.
SOMA UJUMBE WOTE HAPA
Jana Agosti 20,2020 Kikao Cha Halmashauri Kuu Kuu Ya CCM Taifa (NEC) kilimtangaza ndugu Patrobas Katambi kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini uchaguzi Mkuu 2020.
Social Plugin