Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HATIMAYE MRISHO MPOTO 'MJOMBA' AANZA KUVAA VIATU...AELEZA ALIVYOITWA MCHAWI


Msanii wa mashairi Tanzania Mrisho Mpoto

Msanii wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto "Mjomba", ameshea picha mitandaoni ikimuonesha akiwa amevaa viatu huku akiuliza mashabiki zake kwamba aendelee kuvaa viatu au abaki kuwa peku.

Katika picha hiyo ambayo amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ameshaitwa mchawi, mshirikina kwa sababu ya imani yake ya kutembea peku.

"Nimeitwa mchawi, mshirikina na masharti ya mganga kwa kutembea peku, hapo je nirudi peku au nibaki huku" ameandika Mrisho Mpoto.

Ikumbukwe tu msanii huyo alijizolea umaarufu kutokana na style ya kutembea peku popote pale utakapomuona iwe mtaani, studio, mikutano hata akiwa stejini akifanya show na shughuli zingine za kimuziki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com