Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Cecilia Augustino Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini kuwa mgombea urais wa Tanzania na Tabu Mussa Juma mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.
Cecilia ameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage ofisi za tume hiyo zilizopo Dodoma.
Cecilia amekuwa mgombea wa tano kuteuliwa kati ya 17 waliochukua fomu za uteuzi NEC.
Wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Leopard Mahona wa NRA, John Shibuda wa chama cha Ada Tadea na Mutamwega Mgaiwa wa SAU
Cecilia ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kugombea mwaka huu kati ya wawili waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo ya juu.
Mwingine aliyechukua fomu ni; Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC.
Social Plugin