Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akionyesha jezi maalum zilizotolewa na Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd zitakazotumiwa na timu ya Shinyanga Super Queens kwenye mashindano mbalimbali ambazo zimezinduliwa leo katika uwanja wa CCM Kambarage.
Na Damian Masyenene –Shinyanga
Maandalizi ya wawakilishi pekee wa soka la Wanawake mkoa wa Shinyanga, Shinyanga Super Queens yanazidi kupamba moto kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (WFDL) inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Shinyanga Super Queens baada ya kuangukia pua katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya ES Unyanyembe ya Tabora kwa kutandikwa mabao 5-3 kwenye dimba la CCM Kambarage, mjini Shinyanga, leo Jumapili walijitupa tena uwanjani hapo kujaribu makali yake na silaha mpya walizozipata ambapo wamewakaribisha Vijana wenye umri chini ya miaka 17 wa Kituo cha Soka cha Moroto cha mjini Shinyanga, na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mchezo huo ambao ulikuwa maalum kwa ajili ya tukio la uzinduzi wa jezi zao mpya walizokabidhiwa kutoka Kampuni ya Jambo Food Products Ltd , umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko na baadhi ya viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwemo Mkurugenzi wa Shirika Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama.
Mabao yote ya Shinyanga Super Queens yalipachikwa nyavuni na mshambuliaji wao, Irene Chitanda (Messi).
Baada ya mchezo huo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko aliwapongeza viongozi wa timu hiyo kwa kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wa kike na kuwataka waendelee kukazania mazoezi ili kuwa imara zaidi.
Pia Mboneko aliahidi kuwakabidhi Mbuzi (mnyama) wawili na Sh 100,000 kwa ajili ya safari yao ya maandalizi, huku akiahidi Mbuzi mmoja kwa timu ya Moroto FC.
Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti amewashukuru wadau wote amabo wameendelea kuisaidia na kuinga mkono timu yake katika maandalizi hayo ya michuano ya ligi daraja la kwanza, huku akiendelea kuwakaribisha wananchi kuunga mkono safari yao ya kuelekea kwenye michuano hiyo.
Kwa upande wa kampuni ya Jambo Food Products Ltd ambao ndiyo wadhamini wa jezi za Shinyanga Super Queens, kupitia kwa Afisa Masoko wake, Ophebia Juvenary wameahidi kujitolea vinywaji na maji kwa timu hiyo kwa kila mchezo watakaocheza.
Naye Ofisa Michezo na Utamaduni wa Halmashauri ya Shinyanga, Mankiligo alitoa Sh 20,000 kwa timu hizo, huku Jonathan Manyama akitoa Kisanduku cha dawa chenye thamani ya Sh 50,000 na Mbuzi mmoja kwa timu ya Shinyanga Super Queens na Sh 10,000 kwa Moroto FC.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi maalum zilizotolewa na Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd zitakazotumiwa na timu ya Shinyanga Super Queens kwenye mashindano mbalimbali leo katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Afisa Masoko wa Jambo Food Products, Ophebia Juvenary akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi maalum zilizotolewa na Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd zitakazotumiwa na timu ya Shinyanga Super Queens kwenye mashindano mbalimbali leo katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ambapo mchezo kati ya Shinyanga Super Queens na Moroto FC umefanyika ambapo Shinyanga Super Queens wameibuka kidedea kwa kuichapa Moroto Fc bao 2-1.
Kikosi cha Shinyanga Super Queens
Kikosi cha akiba cha Shinyanga Super Queens
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga mpira kuelekea golini kuashiria ufunguzi wa mchezo huo
Beki wa timu ya Shinyanga Super Queens akijaribu kuondoa mpira kwenye eneo lake wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Nahodha wa Shinyanga Super Queens, Tatu Abbas akiwatoka wachezaji wa Moroto FC katika mchezo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo
Mchezaji wa Moroto FC akiwatoka wachezaji wa Shinyanga Super Queens
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiserebuka na wachezaji wa timu ya Shinyanga Super Queens baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vijana wa kiume wa kituo cha Moroto Academy cha mjini Shinyanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Shinyanga Super Queens
Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti akizungumza
Furaha ikiwa imetawala kwa timu ya Shinyanga Super Queens
Via Shinyanga Press Club Blog
Social Plugin