Mkurugenzi Mtendaji Shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala.
***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajumbe wa Kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wametakiwa kuongeza ubunifu zaidi katika kufuatilia taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajumbe wa Kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wametakiwa kuongeza ubunifu zaidi katika kufuatilia taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.
Hayo
yamesemwa leo Ijumaa Agosti 7,2020 na Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Beda
Kamara kwenye kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilicholenga kujadili namna ya kuratibu
utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Kikao
hicho kilichoandaliwa na shirika la The Voice of Marginalized Community (TVMC)
pia kililenga kujadili namna ya Kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata kufanya kazi kwa
kushirikiana na taasisi zingine zinazotoa huduma za jamii sambamba na kuifanya
jamii kumiliki na kuendeleza MTAKUWWA.
Akifungua
kikao hicho, Afisa Tawala huyo wa wilaya ya Shinyanga, aliyemwakilisha Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko alisema ni vyema Wajumbe wa kamati za
MTAKUWWA wakaongeza ubunifu kuwafikia walengwa wakiwemo watoto ili kukabiliana
na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Wajumbe wa Kamati za MTAKUWWA tuongeze mbinu za kutafuta taarifa
kwani kuna vitendo vya ukatili havionekani kwa haraka kama ilivyo m imba lakini
kuna ukatili hauonekani lakini unaumiza. Kuna familia nyingi zinakutana na
ukatili wa kiuchumi. Hebu tuone namna ya kupata taarifa za kutosha ili kupata
mbinu za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,aliongeza Beda.
Aliwashauri
wajumbe hao wa MTAKUWWA kukutana na viongozi wa vitongoji ili kupata taarifa
mbalimbali za masuala ya ukatili wa kijinsia na kutumia mabonanza ya michezo
ili kuibua vipaji na kuibua hisia na changamoto zinazowakabili watoto.
Katika
hatua nyingine Beda alisema suala la utetezi wa haki za wanawake na watoto ni
la kila mmoja katika jamii hivyo ni vyema kila mtu achukue hatua pale anapoona
kuna vitendo vya ukatili vinafanyika.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala alisema shirika
lake limeendelea kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za MTAKUWWA katika kata
saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo ni Samuye, Usanda, Tinde,
Nsalala, Didia, Masengwa na Ilola ambako TVMC inatekeleza Mradi wa kupinga
ukatili wa kijinsia kwa ufadhili wa shirika la Foundation For Civil Society.
“Kikao hiki cha leo ni mwendelezo wa Shirika la TVMC kuendesha
majadiliano na kamati za MTAKUWWA kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia ili
kuhakikisha kamati hizi zifanye kazi kwa ufanisi zaidi. Tumeenda kwenye kata 7
za halmashauri ya Shinyanga na tuna mpango wa kuzifikia kata zingine”,alisema Ngangala.
Kaimu
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omari alisema
hali ya wazazi na walezi kutowajibika katika malezi na makuzi ni miongoni mwa
sababu zinazochangia uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Aidha
alieleza kuwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga imeendelea kutoa elimu ya
masuala ya malezi na makuzi,jinsia na kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia
vikundi vya akina na mama,vijana na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kiuchumi.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini, Grace Salia aliwataka wananchi kuacha
tabia ya kuficha matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
huku akiwahamasisha kujitokeza kutoa ushahidi kwenye kesi zinazohusu ukatili
ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Nao
washiriki wa kikao hicho walisema uwepo wa klabu za wanafunzi shuleni zimekuwa
msaada mkubwa katika upatikanaji wa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto ambapo watoto wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa.
“Kamati za MTAKUWWA zinafanya kazi nzuri na ufuatiliaji umekuwa
mzuri na hizi klabu za watoto shuleni zimekuwa msaada mkubwa kwani watoto
wenyewe sasa wanatoa taarifa za matukio ya ukatili”,alisema Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Usanda,
Halima Tendega.
Kikao
hicho kimekutanisha pamoja viongozi wa Kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata,
Watendaji wa kata na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwemo
Mwanasheria,Afisa Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii, Mganga
Mkuu,Hakimu,Polisi, Maafisa Elimu na maafisa kutoka shirika la TVMC ambapo
wakati wa kikao hicho wajumbe wa kila kata walitengeneza Mpango kazi wa
kutekeleza MTAKUWWA.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoandaliwa na shirika la TVMC kwa lengo la kujadili namna ya kuratibu utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akisisitiza umuhimu wa kamati za MTAKUWWA kuongeza mbinu zaidi za kutafuta taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini,Grace Salia akifuatiwa na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Janeth Elias.
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akizungumza katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoandaliwa na shirika la TVMC kwa lengo la kujadili namna ya kuratibu utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akifafanua namna shirika la TVMC linavyoshirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akiwahamasisha wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kuendelea kutoa t
Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Asha Omari akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini, Grace Salia akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Janeth Elias akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Washiriki wa kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye Ibrahimu Bundo akiwasilisha taarifa kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika kata ya Samuye.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Shinyanga, Opeyo Sisso akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Msingi wilaya ya Shinyanga, Joseph Bihemo akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Kaimu Mganga Mkuu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Dkt. Mushi Fidelis akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwanasheria halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Salehe Hassan akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwakilishi wa Hakimu mahakama ya Mwanzo Usanda,Judith Mnyasi akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Happiness Misael Shao akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Didia Felister Jonathan Melli akitoa taarifa ya matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika kata ya Didia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye Ibrahimu Bundo akiwasilisha taarifa kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika kata ya Samuye.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Shinyanga, Opeyo Sisso akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Msingi wilaya ya Shinyanga, Joseph Bihemo akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Kaimu Mganga Mkuu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Dkt. Mushi Fidelis akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwanasheria halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Salehe Hassan akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mwakilishi wa Hakimu mahakama ya Mwanzo Usanda,Judith Mnyasi akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Happiness Misael Shao akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Washiriki wa kikao wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog