Picha : TVMC WAFANYA BONANZA LA MICHEZO WANAFUNZI DIDIA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la TVMC linalotetea haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga limefanya Bonanza la michezo kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Bonanza hilo limefanyika leo, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari DonBosco, na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu, watendaji wa Kata, vijiji, Maofisa Ustawi wa jamii, Maendeleo, pamoja na dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi, kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.

Shule zilizohudhuria Bonanza hilo ni Shule ya Msingi Didia, Bugisi, Mwamalulu, Mwanono, Bukumbi, pamoja na Ola, huku Shule za Sekondari ni Didia na DonBosco.

Akizungumza kwenye bonanza hilo Mkurugenzi wa Shirika TVMC Musa Ngangala, amesema Bonanza hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wao wa kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwenye Kata hiyo ya Didia.

Amesema moja ya njia ya kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ni kuendesha mabonanza ya michezo ambayo hukusanya wanafunzi wengi kwa wakati moja.

"Dhumuni la kufanya Bonanza hili la michezo ni kufikisha ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili ndani ya jamii, dhidi ya wanawake na watoto, ili kuifanya jamii iwe salama," amesema Ngangala.

"Vitendo vya ukatili ambavyo tunavipinga, ni vipigo kwa wanawake, na watoto, utumikishaji watoto, kuwanyima haki ya kupata elimu, pamoja na tatizo la mimba na ndoa za utotoni," ameongeza.

Pia Ngangala amewataka wanafunzi kupaza sauti pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili, na siyo kukaa kimya, ili wahusika wachukuliwe hatua kali, jambo ambalo litatokomeza matukio hayo.

Naye mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala, akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Jasinta Mboneko, amewataka wanafunzi hasa wa kike, wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao ,pamoja na kukataa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala, akizungumza kwenye kongamano hilo.

Afisa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Opeyo Sisso, akizungumza kwenye Bonanza hilo na kuwataka wanafunzi wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao.

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Musa Ngangala, akizungumza kwenye Kongamano hilo na kuwataka wanafunzi wapaze sauti za ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa ili wahusika wachukuliwe hatua.

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Musa Ngangala, akielezea madhumuni ya Bonanza hilo la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Wanafunzi wakisikiliza nasaha wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo la michezo la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Wanafunzi wakisikiliza nasaha wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo la michezo la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akifungua Bonanza hilo.

Bonanza la michezo likianza kwa  riadha.

Wanafunzi wakifukuza kuku, ambapo mshindi umeondoka na kuku huyo.

Zoezi la ufukuzaji kuku likiendelea.

Wanafunzi wakishindana kukimbia kwa kuvaa magunia.

Wanafunzi wakishindana kukimbia kwa kuvaa magunia.

Wanafunzi wakicheza mpira wa Pete.

Wanafunzi wakicheza mpira wa wavu.

Mpira wa kikapu ukiendelea kuchezwa.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Didia jezi (Nyeusi), pamoja na Wanafunzi wa shule ya Sekondari DonBosco( Jezi ya Orange), wakitoa Burudani kwenye Bonanza hilo la michezo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Didia,( Jezi Nyekundu) na Mwanono (Jezi Nyeupe na mistari nyeusi wakitoa burudani kwenye bonanza hilo.

Burudani ya mpira wa miguu ikiendelea kutolewa.

Penalti zikipigwa mara baada ya Timu za DonBosco na Didia Sekondari kutoka bila ya kufungana.

Penalti zikipigwa mara baada ya Timu za DonBosco na Didia Sekondari kutoka bila ya kufungana, ambapo katika Penalti hizo, Timu ya Didia Sekondari waliibuka na Ushindi.

Wanafunzi wakiwa kwenye Bonanza wakitazama michezo mbalimbali ikichezwa.

Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala, akigawa zawadi mbalimbali kwa washindi katika Bonanza hilo la Michezo.

Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala, akigawa zawadi mbalimbali kwa washindi katika Bonanza hilo la Michezo lililoandaliwa na Shirika la TVMC kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post