Kushoto ni Mgombea Urais wa Zanzibar Maalim Seif na kulia ni Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Membe.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, wamempitisha Mshauri Mkuu wa chama hicho Bernard Membe, kupeperusha bendera ya chama hicho katika kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maamuzi hayo yameamuliwa hii leo Agosti 5, 2020, wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Membe ameibuka mshindi kwa kupata kura 410 kati ya kura 420.
Aidha Wajumbe wa mkutano huo pia wamempitisha Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, baada ya kupata kura 419 kati ya kura 420.
Social Plugin