Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imetangaza wateule wa nafasi za Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 huku jina la Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda likikatwa.
Muda mchache baada ya zoezi hilo kumalizika Makonda ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hata kama maombi yake hayajajibiwa, atabaki kumwamini Mungu wake
“Nina mwabudu Mungu aliye hai. Hata asipo jibu sawa na maombi yangu, bado atabaki kuwa Mungu wangu”- Paul Makonda
Social Plugin