Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Melchedes Burchard (30) mkazi wa Kiluluma mkoani Kagera kwa kukutwa na hatia ya kumuua kikatili mtoto wake mwenye umri wa miaka 2 na nusu witness melchedes kwa kumkata mapanga kisha kutenganisha kichwa chake na kiwiliwili kwa madai kuwa mke wake alimzaa nje ya ndoa.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Lucia Kairo ambapo amesema vitendo vya mauaji vinavyoendelea kushika kasi mkoni Kagera hususani kati ya wanandoa na watoto ambao hawana hatia kuwa vinahatarisha usalama na amani hivyo mahakama itaendelea kutoa adhabu kali kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo .
Melchedes alifanya mauaji hayo ya kikatili ya mtoto huyo Julai 27, 2015, katika tukio hilo baada ya kukata mapanga mtoto huyo alimficha kwenye kichaka kilichoko karibu na nyumba yake na alipomaliza kufanya hivyo alirudi ndani ya nyumba yake na kuendelea na shughuli zake.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili wa serikali Haruna Shomari amesema kuwa ameridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama kwa kuwa itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia ambazo sio za kibinadamu.
Social Plugin