Mshambuaji ambaye aliwauwa kwa bunduki waumini 51 kwenye misikiti miwili nchini New Zealand amehukumiwa kifungo cha maisha jela na kwa sharti kwamba muda wa kifungo hicho hauwezi kupunguzwa.
Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo ambayo ndiyo ya juu zaidi na ya kwanza ya kutolewa nchini New Zealand inalenga kuonesha jinsi matendo ya mshambuliaji huyo Brenton Tarrant yalivyokosa utu.
Jaji Mander ameongeza kusema kuwa makosa yaliyofanywa na mwanaume huyo raia wa Australia ni ukatili wa kiwango kibaya ambao hata hukumu ya maisha jela haiwezi kufuta hasara na maumivu aliyosababisha.
Katika mashambulizi ya Machi 2019, Tarrant aliwashambulia kwa bunduki za rashasha waumini waliokuwa kwenye ibada katika msikiti wa Al Noor na Linwoood mjini Christchurch.
Tangu Machi mwaka huu Tarrant alikubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, mshambuliaji huyo alisema anakiri kuwa na hatia ya kuwauwa waumini 51 na jaribio la kuwauwa wengine 40 katika mashambulizi ya bunduki aliyoyafanya mwezi Machi mwaka 2019.
Social Plugin