Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema Bernard Morrison ameshinda kesi yake dhidi ya Yanga Sc na ataendelea kuwa mchezaji halali wa Simba Sc baada ya mapungufu kukutwa kwenye mkataba baina ya Yanga Sc na Morrison.
"Mapungufu makubwa ambayo tumeyaona ni tarehe ya mkataba, tarehe ya mkataba inaonesha ilisainiwa Machi 20, 2020 wakati tarehe sahihi inaonesha Julai 17, 2020 pia ukurasa wa kutia sahihi umekatwa"- Elias Mwanjala, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Wachezaji
Social Plugin