Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BRELA YASHIRIKI MAONYESHO YA KITAIFA NANENANE MKOANI LINDI

Team ya Brela ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Ally Mketo wa pili kutoka kushoto wakiwa tayari Banda leo kutoa huduma
Afisa kutoka Brela Bi Sada Kilabula kulia akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
WAKALA wa  usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki maonyesho ya wakulima nane nane kwenye mikoa ya Simiyu na Lindi ili kuweza kuwafikia zaidi wananchi wake katika utoaji wa elimu ya kurasimisha biashara na huduma zinazotolewa na wakala huo.

BRELA ni Taasisi  iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo jukumu la taasisi ni kusajili majina ya Biashara, makampuni, nembo za huduma na biashara, Hataza, Utoaji wa leseni za Biashara daraja A na Leseni za Viwanda.

Katika Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho hayo wakala huo uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha Bakari Mketo ambaye alibainisha kwamba lengo kuu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma na utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wakati wa kufanya sajili mbalimbali za BRELA papo kwa papo.

Pamoja na yote amewataka wakulima na wadau mbalimbali kuweza kurasimisha biashara zao ili kutambulika na kuweza kuufikia Uchumi wa kati.

Pia ameeleza kwamba dhumuni la kushiriki maonesho ni kuwasogezea wananchi wa lindi huduma kwa ukaribu na kuendelea kutoa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatembelea katika banda lao lililopo katika viwanja vya Ngongo ili kuweza kupata huduma za sajili papo kwa papo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com